Posts

Showing posts from April, 2017

Huyu Ndiye Mtoto Mtanzania Anayeaemekana Kuwa na Uelewa na Ujuzi wa Hali ya Juu.

# Ithan #Mahafudh , ni mtoto mwenye umri wa miaka mitatu, ameendelea kuthibitisha #kipaji kikubwa alichonacho, akiwa na uwezo wa kuwataja karibu marais wa nchi zote duniani ambapo #Pasaka hii, alikuwa kivutio kwenye #event iliyoandaliwa na #Shilawadu ambapo alijibu maswali yote ya papo kwa hapo. Mtoto huyo, licha ya uwezo wake wa kutaja majina ya viongozi mbalimbali, anao uwezo mkubwa wa kukariri mambo mengi kwa wakati mmoja. Mtazame zaidi hapa...         http:// bit.ly /2oOwCko Maajabu mengine ya mtoto Ithan ni kuwa anafahamu kuendesha gari na pia anajua kutumia kompyuta na simu za kisasa yaani smartphones, kwani anao uwezo wa kuingia katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Serikali Yawapandisha Watumishi 2000 Vyeo

Watumishi 2,000 Elimu wapandishwa V yeo WAZIRI WA ELIMU, PROFESA JOYCE NDALICHAKO . BUNGE limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapandisha daraja wale waliostahili na kuwa lini itawalipa madai yao ya fedha za likizo ambazo watumishi hawajalipwa kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kuzipata kwa wakati. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alibainisha serikali inaendelea kulipa madeni, ikiwamo fedha za likizo kwa walimu au watumishi katika sekta ya Elimu, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi Juni 2016, jumla ya Sh. Bilioni  22.7 zililipwa kwa walimu 63,814. Aidha, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/17 h

Machache Kuhusu Korea Kaskazini(North Korea).

MACHACHE ZAIDI KUHUSU KOREA KASKAZINI . 1. Bangi ni Halali kabisa nchi nzima, na haichukuliwi kama ni kitu cha kulewesha yaani Drug. 2. Ndio nchi pekee duniani hadi sasa ambayo imewahi kuiteka meli ya kivita ya wamarekani. 3. Wakati dunia nzima leo ni 2017 kwao ni mwaka 106 wakihesabu kuanzia kifo cha kiongozi wao Kim il-Sung-.Baba wa taifa lao Kim II-Sung alizaliwa 15.04.1912 siku ilipozama meli ya Titanic . (Rais wa Maisha wa Korea Kaskazini ni Kim Il Sung. Mtoto wake na mjukuu wake wamekuja kuwa viongozi tu, lakini yeye mwenyewe babu yao ndiye rais mpaka leo, hata kama amefariki.....Eternal President of the Republic-Hayo ndiyo mambo ya North Korea).    Hiyo siku ndio chanzo cha kalenda yao (Democratic People's Republic of Korea_Juche Korea[/QUOTE] year Gregorian year Dangun year-Kim alizaliwa 1912 ~ hapa ndio juche year inaanzia). 4. Kuanzia 2009 nchi hii sio ya kikomunist tena, wana msimamo au IDEOLOGY yaoo mpya unaitwa " JUCHE " wakimaanisha " KU

Aliyoyasema Mwigulu Nchemba Kuhusu Mauwaji ya Askari Nane.

Mwigulu Nchemba baada ya kutembelea eneo walilouawa Askari Nane . Wakati jioni ya April 13 2017 Wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, iliripotiwa kuwa watu wanaosadikika kuwa majambazi ambao haijafahamika idadi yao wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la polisi na kuwaua askari nane na kumjeruhi mmoja Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba   leo April 14 2017 ametembelea eneo lilipotokea tukio la mauaji ya Askari nane wa Jeshi la Polisi na kusema kuwa waliotekeleza mauaji hayo watalipa damu ya akari hao iliyomwagika.

Maamuzi ya Canada Kuhusu Bangi Itakapofikia 2018 Ni haya.

Kufikia 2018 haya ndiyo maamuzi watakayofikia Canada kuhusu Bangi. Kadiri siku zinavyobadilika na miaka kusonga mbele ndivyo nchi mbalimbali duniani hufanya marekebisho katika sheria za nchi kulingana na hitajio la wananchi kwa maendeleo ya Taifa. Leo April 14, 2017 mtandao maarufu wa CNN umeripoti taarifa kuhusu mpango wa Serikali ya Canada chini ya Waziri Mkuu Justin Trudeau kuweka wazi mipango yake ya kuhalalisha bangi ifikapo 2018 ambapo kama Bunge la nchi hiyo litapitisha muswada huo, Canada itakuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kuhalalisha soko la bangi. Waziri Mkuu aliandika kwenye account yake ya Twitter: “ Ni rahisi sana kwa watoto wetu kupata bangi. Tutaibadilisha.“ – Justin Trudeau . Licha ya kutaka kuhalalisha bangi, pia yametajwa mambo matano ya kuyafahamu kuhusu pendekezo la Canada katika sera ya bangi ambayo rasmi itakuwa July 2018. 1: Serikali kusimamia mauzo ya bangi Serikali ya Canada itaweka mfumo maalum wa kuzalisha, kusambaza na kuuza bangi am

Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Mauwaji ya Askari Nane.

Kauli ya Jeshi la Polisi kuhusu mauaji ya askari polisi nane . Jana April 13 2017 jioni Wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, iliripotiwa kuwa watu wanaosadikika kuwa majambazi ambao haijafahamika idadi yao wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la polisi na kuwaua askari nane na kumjeruhi mmoja. Leo April 14 2017 katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo , Nsato Marijani amesema katika tukio hilo majambazi hao walipora silaha saba ; SMG nne na Lon Range tatu. Aidha, Marijani amesema mara baada ya tukio hilo, hatua za kiintelijensia na kipelelezi ambazo zilichukuliwa askari kufuatilia, zilibaini maficho ya muda ya majambazi hao ambapo katika majibizano ya risasi majambazi wanne waliuawa na bunduki nne kupatikana hivyo amesema kuanzia sasa Jeshi la Polisi linakwenda kwenye oparesheni maalumu kupambana na majambazi hao.

Raisi John P.Magufuli Ampigia Simu Nwana FA na Kumpongeza.

Image
Jioni ya April 12 2017 staa wa muziki wa hip hop bongo Hamisi Mwinjuma ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la Mwana FA, alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuoneshwa kufurahisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kumpigia simu. Mwana FA ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika radio na tv stations mbambali kwa hit single yake ya Dume Suruali amethibitisha kupigiwa simu na Rais kumwambi anakubali kazi zake. Kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa staa huyo uliyokuwa verified aliandika “nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais @ MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa # DumeSuruali ..

Serikali yatangaza majina ya Ajira za Ualimu.

BREAKING NEWS: HAYA HAPA MAJINA AJIRA MPYA ZA WALIMU 2016/2017. Hatimaye serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza majina ya walimu walioajiriwa mwaka katika Ngazi ya Stashahada wa Mwaka 2016/2017           Bonyeza hapa kuyatazama .

Walicholisema Stamina na Bill Bass kuhusiana na utekaji huku wakiitambulisha Ngoma Yao Mpya.

Stamina na Bill Nass wamezungumzia kuhusu utekaji . Leo April 12 2017 kupitia kwenye XXL ya Clouds FM wakali kutoka Bongoflevani Bill Nass na Stamina wamezungumzia kuhusu vitendo vya utekaji watu baada ya Roma Mkatoliki na wenzake watatu kutekwa na watu wasiojulikana kabla ya kuonekana. Stamina amedai kuwa haoni sababu nyingine zaidi ya muziki ambao umekuwa hukisababisha utekaji hivyo kuwanyima uhuru wa sanaa, huku Bill Nass akisema hatumii muda mwingi kutoka nje kabla na  baada ya saa sita usiku kuhofia kutekwa. >>>“ Sioni kama kuna kitu kingine zaidi ya muziki. Ndiyo sababu nayaona matukio ya utekaji kama ni kutunyima uhuru wa sanaa yetu ." - Stamina . >>>” Siku hizi situmii muda mwingi nje. Watu wangu wa karibu wanapenda niwepo ndani kabla ya saa sita usiku juu ya hofu ya utekaji. ” - Billnass . Bill Nass na Stamina wamezitoa kauli hizo wakati wakiutambulisha wimbo wao mpya unaoitwa Aje mwenyewe walioshirikiana wasanii watatu ambao

RFEF Imemfungia Neymar Mechi tatu mfululizo.

BAD NEWS: RFEF imemfungia Neymar leo April 11 2017. Staa wa soka wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Neymar amekutana na adhabu ya kufungiwa mechi 3 mfululizo  kuichezea FC Barcelona na shirikisho la soka Hispania ( Royal Spanish Football Federation (RFEF) kwa makosa mawili. Neymar amefungiwa mechi tatu, mechi moja ni kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano wakati wa mchezo dhidi ya Malaga uliyomalizika kwa FC Barcelona kupoteza kwa magoli mawili kwa 2-0 lakini mechi ya mbili kwa kosa la kumpongeza kwa kejeli fourth official wakati anatoka nje ya uwanja. Neymar alipooneshwa kadi ya pili ya njano, Mchezaji huyo raia wa Brazil alitoa lugha za kejeli kwa fourth official wakati anatoka uwanjani kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano, refa wa game hiyo Jesus Gil Manzano ndio aliandika ripoti hiyo, Neymar sasa atakosa mchezo dhidi ya Real Sociedad, Real Madrid na Osasuna.

Wajumbe Walioapishwa na Mheshimiwa Raisi ili kwenda kufanya Uchunguzi wa Makontena yaliotoka nchini Tangu Mwaka 1998.

Rais Maghufuli amewaapisha Wajumbe wa Kamati Maalumu . Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo April 11, 2017 amewaapisha Wajumbe wa Kamati Maalum ya pili ya wachumi na wanasheria ambayo itachunguza mchanga wenye madini uliomo kwenye makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini. Wajumbe walioapishwa ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Nehemiah Eliachim Osoro na wajumbe wake ambao ni Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara, Dkt. Oswald Joseph Mashindano, Bw. Casmir Sumba Kyuki, Bw. Andrew Wilson Massawe na Bw. Gabriel Pascal Malata . Wengine ni Bw. Usaje Bernard Usubisye na Bi. Butamo Kasuka Philip ambapo baada ya kuwaapisha wajumbe hao Rais Magufuli amesema ameunda kamati hiyo ili ifanye uchunguzi wa kina utakaobaini aina ya madini yaliyomo ndani ya mchanga huo, thamani yake, kiwango cha kila aina ya madini, uzito wa mchanga unaowekwa ndani ya makontena na kujua ni makontena mangapi yamepitishwa tangu mwaka 1998. “ Kafuatilieni makontena mangapi yametoka hapa nchini na kupelekwa

Sifa za wanaotakiwa kujiunga na Mafunzo ya Afya Ngazi ya Cheti na Stashahada(Diploma).

Kwa wale wanaohitaji kutumq mombi kwa ajili ya mafunzo ingia link hii hapa chini ili kuweza kutazama Sifa za waombaji mafunzo ya Afya katika Ngazi za Cheti na Stashahada yaani Diploma. http:// maswayetu.blogspot.nl /2017/04/ taarifa-muhimu-kuhusu-sifa-za-kujiunga.html .

Viwanja Kumi Bora Afrika,Ukanda wa Mashariki Upo mmoja tu.

TOP 10 ya viwanja ghali zaidi Afrika , Afrika Mashariki upo mmoja . Licha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF kusema moja ya sababu kuu inayopelekea Bara la Africa kufanya vibaya kwenye mchezo wa mpira wa miguu duniani ni ukosefu wa viwanja bora, kuna baadhi ya nchi Afrika zina viwanja vizuri na vyenye gharama kubwa ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea. Leo April 10, 2017 nimekuletea list ya viwanja 10 vizuri na vyenye gharama zaidi barani Afrika hadi kufikia December 2016. 1: Capetown Stadium, Afrika Kusini Uwanja huu una uwezo wa kuingiza mashabiki 64,100 ambapo umejengwa na kampuni ya Afrika Kusini ukiigharimu nchi hiyo Dollar 600 million ukiwa ndiyo uwanja wenye gharama kwa Afrika. 2: Moses Madiba Stadium, Afrika Kusini Moses Madiba ulikuwa moja ya viwanja vilivyotumika wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2010 ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 62,760. Uligharimu Dollar 450 million. 3: FNB Stadium, Afrika Kusini Uwanja huu unashikilia rekodi ya

Tamko la Waziri Kuhusu Bonde la Mto Ruaha.

Tamko la waziri Makamba kuhusu bonde la Mto Ruaha . Jumapili ya April 9 2017 waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais-muungano na mazingira January Makamba aliamua kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza mpango wake wa kuzindua kikosi kazi cha kitaifa kuhusu bonde la M to Ruaha mkuu Iringa . Mpango huo ambao makamu wa Rais na mawaziri watano wataelekea Iringa siku ya Jumanne ya April 11 2017 lengo likiwa ni kukagua na kuangalia bonde la mto Ruaha ambalo linakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira hususani wa ardhi. Uharibifu wa mazingira katika bonde la mto Ruaha kwa kiasi kikubwa unatokana na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu zinazofanywa katika maeneo ya vyanzo vya maji pamoja na vilele vya milima, miteremko ya milima na katika mabonde. Baada ya kugundua uharibifu huo unaoendelea kufanyika katika bonde la mto Ruaha, serikali kwa kushirikiana na wadau imeona kuna haja ya kuwa na mtazamo mpya wa namna ya kukabiliana na changamoto za mto Ruaha Mkuu kwa ufa

Lau Wa John Feat Lee Classic & Zilly-Usijari.

Sikiliza wimbo mpya kutoka kwa Lau wa John Feat Lee Classic & Zilly- Usijari . Bofya hapa chini kuupakua na kuusikiliza pia. http://www.djmwanga.com/2017/03/lau-wa-john-x-lee-classic-x-zilly-usijari.html?m=1

To those who wants to Make and Earn Money Online.

Please follow the Link below in order to be directed on how to get paid when you share your link with your family members. http:// dollarsaw.com /?share=154803 Usikose kutembelea www . dbmclassic . blogspot . com / Kila mara ili kupata taarifa mbalimbali.

Nchi Ishirini Zinazoongoza kwa Mabilionea.

DUNIANI TOP 20 ya nchi zenye Mabilionea wengi zaidi Duniai . Baada ya Shirika la Fedha duniani ‘IMF’ kutangaza kuongezeka kwa uchumi wa dunia ukilinganisha na mwaka 2016, taarifa iliyoweza kutolewa April 8 2017 ikionesha list ya nchi zenye mabilionea wengi zaidi duniani kwa mwaka 2017, kwa mujibu wa tovuti ya takwimu Statista . Takwimu hizi zinaonesha kuwa;- 1.China ndiyo nchi yenye mabilionea wengi duniani ambao ni zaidi ya 609. 2.kifuatiwa na Marekani yenye mabilionea 552. 3.Ujerumani-109. 4.India-100. 5.Uingereza-89. 6.Uswizi-77. 7.Urusi-68. 8.Ufaransa-50. 9.Brazili-43. 10.Japani-42. 11.Italia-41. 12.Kanada-35. 13.Korea Kusini-34. 14.Uturuki-29. 15.Singapo-28. 16.Australia-27. 17.Tailendi-26. 18.Hispania-23. 19.Jamhuri ya Nchi za Kiarabu(U.A.E)-21. 20.Indonesia-17. Katika list hii Sweden inakamata nafasi ya mwisho ikiwa na mabilionea 17.

Roma, three Colleagues found Bruised (Strike):Lawyer.

Roma, three colleagues found bruised: lawyer . Hip hop star Ibrahim Musa a.k.a Roma Mkatoliki . @TheCitizenTz. Dar es Salaam. Hip hop star Ibrahim Musa a.k.a Roma Mkatoliki and his three colleagues who went missing on Wednesday evening after a suspected abduction were yesterday found alive in undisclosed locations and circumstances. Speaking from Mwananyamala Referral Hospital where he and the three had been taken for treatment, Roma said : “I thank Tanzanians for their support. I’m well but I can’t talk more for now. I’m waiting for police procedures. ” He promised to hold a press conference tomorrow and divulge details ". By noon yesterday, Dar es Salaam Special Zone police commander Simon Sirro told the press that the whereabouts of Roma and his colleagues was unknown. However, about an hour later, it came to light that the artistes had been found and were at the Oysterbay Police Station. However, journalists were barred from interviewing them and by 6pm, Roma’s lawyer

Roma Aongea kwa mara ya lwanza baada ya kurudi Uraiani.

MIX VIDEO: Roma aongea kwa mara ya kwanza baada ya kurudi uraiani By Millard Ayo. Msanii wa Bongofleva Roma Mkatoliki na wenzake watatu wamerudi uraiani baada ya kuripotiwa kutekwa April 5 2017 na kupelekwa kusikojulikana, baada ya kurudi uraiani ameyaongea haya hapa chini. " Siwezi kuongea mengi maana tunahitaji muda wa kupumzika nopende kuwaambia watanzania wote mimi ni mzima pamoja na wenzangu wote watatu Moni , Emma na Bin Laden hivyo pia nipende kuwashukuru watanzania wote kwa support yao japokuwa sijaweza kupita katika mitandao ya kijamii pia niweze lumshukuru ndugu Ruge Mtaaba kwa ushirikiano wake tangu asubuhi tumekuwa naye "

Breaking News.

Taarifa zilizopo zinazohusu Roma alipo . Taarifa ambazo zimetolewa leo mchana na mmiliki wa Studio ya TONGWE zinasema kuwa Roma na wenzake ambao waliotekwa wameweza kujulikanaahali walipo amnapo ameweza kutaja kuwa Roma na wenzake wapo katika kituo cha Osterbay . Taarifa zaidi nitakusogezea kila inapotokea mahali au sehemu yoyote ahsante.

Alichokiandika Mbunge Hessein Bashe kuhusu Roma Mkatoliki.

Alichokiandika Mbunge Hussein Bashe kuhusu Roma Mkatoliki By Rama Mwelondo . TZA . Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatoliki zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuripotiwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa Studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana. Watu mbalimbali ikiwemo wasanii mbalimbali wamekuwa wakionesha hisia zao juu ya tukio hilo kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuoneshwa kuguswa na tukio hilo, Mbunge wa Nzega Hussein Bashe ni miongoni mwa watu waliyotumia kuraza zao za instagram kuandika anachowaza kuhusu Roma. Who is behind all this? “ Ni genge ambalo limejipa mamlaka ya kupandikiza woga na chuki miongoni mwa jamii na kuharibu Taswira ya CCM. Tunawajibu wa kukataa woga ,Tunawajibu wa kutoruhusu Misuse ya vyombo vya Ulinzi na usalama, Tunawajibu wa kulinda Taifa letu ” “ Tunawajibu wa kupigania Values zilizopiganiwa na waasisi wa Taifa letu kama Mzee

Maneno Matatu ya Nape Kuhusu kutokuonekana kwa Roma.

Maneno matatu ya Nape Nnauye kuhusu Roma . Baada ya mastaa mbalimbali kuguswa juu ya stori ya Roma mkatoliki na wenzake watatu kuchukuliwa na watu wasiofahamika kwenye Studio za Tongwe Records na kupelekwa sehemu isiyojulikana, sasa leo April 7 2017 Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Moses Nnauye ameonesha hisia zake juu ya tukio hilo. Kupitia account yake ya twitter Nape Nnauye ameyaandika maneno haya matatu kuhusu Roma…>>> ”Roma! Oooooh No! ” -Nape Nnauye.

The Siti Msanii kutoka TONGWE alivyoshuhudia kuchukuliwa kwa Roma.

Shuhuda ameeleza Roma na wenzake walivyochukuliwa Tongwe Records. Zimepita siku mbili tangu staa wa Hip Hop Bongo Roma kuchukuliwa na watu wasiojulikana pamoja na wenzake wakiwa katika studio za Tongwe Records bila kujulikana walikopelekwa, basi leo April 7, 2017 msanii kutoka Tongwe Records ameelezea jinsi watu hao walivyochukuliwa. The Siti ameiambia millardayo.com na Ayo TV jinsi Roma Mkatoliki na wenzake walivyochukuliwa Tongwe Records ambapo hadi sasa haijafahamika mahala walipo na watu waliowachukua . Akizungumza na millardayo.com pamoja na  Ayo TV The Siti alisema:>>> ”Ilitokea kama Jumatano saa kumi na mbili jioni na walikuja watu pale wakashuka kutoka kwenye Noah wakatuambia tuingie ndani ya geti na tukaingia ndani ya geti. Wakamuulizia Junior wakaambiwa hayupo, kisha wakamuulizia na Roma Mkatoliki wakaomba waitiwe Roma kisha walipoitiwa Roma, walimuhoji pale mara wakaingia studio wakachukua vitu na wakawachukua wakina Moni .” -The Siti.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari,Sanaa na Michezo Kuhusu Roma.

Taarifa ya kwanza ya Wizara ya Habari kuhusu kupotea kwa Roma Mkatoliki. Taarifa za kupotea kwa Msanii Roma Mkatoliki na wenzake watatu baada ya kutekwa na kuchukuliwa na Watu wasiojulikana kwenye studio za TONGWE Dar es Salaam, zilianza kusambaa kuanzia juzi usiku (April 5 2017). Leo April 7 2017 Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambayo iko chini ya Dr. Mwakyembe imetoa taarifa ifuatayo >>>> “Kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa, Wizara imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “ Roma Mkatoliki ””. " Wizara imefuatilia kwa karibu suala hili kwa kuwa lina muelekeo wa jinai. Hata hivyo taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi ." Kutokana na hali hiyo, Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.

Maneno ya Nchemba Kuhusu Roma.

Maneno 39 ya Waziri Nchemba kuhusu Roma Mkatoliki . Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatolikia zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuandikwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa Studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni , Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma. “ Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma ” -Nchemba.

Wanasayansi wamegundua Tiba ya Hangover.

Utafiti Mpya kutoka kwa Wanasayansi, wamegundua tiba ya Hangover Hii ni dunia ambayo kila siku watu wanafanya utafiti wa mambo mbaimbali…sasa leo April 7, 2017 nakuletea matokeo ya utafiti uliofanywa na wanafunzi wa wawili nchini Marekani waliogundua tiba ya hangover. Unaambiwa katika stori iliyochapishwa na Daily Mail March 29, 2017, wanafunzi wawili kutoka Yale University wamegundua tiba hiyo ambayo wameapa jina la SunUp ikiwa ni unga uliotokana na mchanganyiko wa viungo vya asili ambao umegunduliwa kwa lengo la kuvunja vunja molikuli za sumu kwenye ini, na kubalansi glutamine pamoja na kuuamsha mwili kwa elektroliti baada ya kunywa pombe. Margaret Morese na Liam McClintock ambao waliathiwa sana na Hangover waligundua tiba hiyo baada ya kujaribu viungo vya asili kila kimoja kivyake katika tafiti huru kuthibitisha uwezo wake dhidi ya kuondoa athari za kilevi na ulinzi thabiti dhidi ya sumu itokanayo na kilevi kwa mtumiaji na baadaye kutengeneza unga huo ambao humtaka mtumiaj

Taarifa Kuhusu Kupotea Kwa Msanii Roma Mkatoliki.

Taarifa zilizopo ni kuwa Msanii Roma Mkatoliki kutokea katika Studio ya Tongwe ( Tongwe Rocords ) alivamiwa na watu wasiojulikana Majira ya Usiku wa kuamkia Siku ya Alhamisi. Msanii huyo alivamiwa Studioni hapo akiwa  studioni hapo na kupelekwa sehemu kusilojulikana pamoja na mwemzake Moni au @ centralzone kama anavyojulikana. Familia ya Msanii Roma ( Mkewe ) ameweza kusema kuwa simu ya Msanii huyo(Mmewe) imekuwa ikiita tu bila kupokelewa hivyo akiwaomba Watanzania wote waweze kumpa ushirikiano wa taarifa zozote za kuhusiana na Msanii Roma (Mmewe) sehemu yoyote ile ambapo zlatapatikana.

Nay Wa Mitego Ametusogezea Wapo video.

Bofya hapa chini kuitizama. http://millardayo.com/po67/

Stori Kumi za Uharifu Zitakazokushangaza Zaidi.

Stori Kumi(10) za wahalifu zitakazokushangaza duniani. Wahalifu wengi hutumia akili nyingi wakati wa kufanya uhalifu ili wasikamatwe au kutiwa nguvuni na vyombo vya dola lakini mara nyingine hujikuta wamefanya makosa madogo madogo ambayo huwakamatisha na kujikuta mikononi mwa sheria. 1: Joseph Martin  Joseph Martin kutokea Florida Marekani alipiga simu Polisi kushitaki baada ya kuagiza bangi na muuzaji kukimbia na pesa yake. Badala ya Polisi kumsaidia shida yake walimtafuta na kumkamata kwa kosa la kutumia mihadarati ambayo imezuiwa kisheria. 2: Tyron Jr Tyron Jr kutokea Carlifornia Marekani alikwenda Mahakamani kusikiliza kesi yake ya wizi wa gari lakini alijikuta akipata kesi mbili baada ya Polisi kugundua gari aina ya Lexus SUV alilokuja nalo Mahakamani hapo aliliiba miezi michache iliyopita kabla ya kukamatwa kwa kesi ya pili. 3: Jonathan Parker Jonathan Parker alivamia nyumba moja katika mji wa Pennsylvania Marekani ambapo baada ya kuiba vitu kadhaa aliamua kuingia kwenye

Mapato yalikusanywa na TRA ndani ya Miezi Tisa.

Mapato ambayo TRA wamekusanya kwa miezi Tisa. Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ imetoa ripoti ya mapato yaliyokusanywa ndani ya miezi 9 kuanzia June 2016 hadi March 2017 ambayo ni Shilingi Trillion 10.87 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.99 ukilinganisha na mwaka uliopita. Akizungmzia makusanyo hayo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo alisema zaidi ya Shilingi Trillion 1.34 zilikusanywa katika mwezi March 2017 pekee ikionesha kupanda kwa asilimia 2.23 ukilinganisha makusanyo ya mwezi kama huo mwaka 2016 ambapo zilikusanywa Shilingi Trillion 1.31.

Wasanii Waliowahi Kuambiwa hawajui kuimba lakini sasa ni Mastaa.

BURUDANI Waimbaji 10 waliowahi kuambiwa hawajui kuimba lakini leo ni mastaa wa Dunia. Mara nyingi watu wanaposhindwa na jambo hukata tamaa lakini kushindwa mara moja haimaanishi huwezi kufanikiwa jambo hilo ukijaribu tena na tena, leo nimekuletea list ya wanamuziki kumi waliowahi kuambiwa hawajui kuimba na leo hii ni mastaa wakubwa duniani. 1: Beyonce . Akiwa na miaka 14 tu alipelekwa na baba yake Mathew Knowles studio lakini producer alipomsikia Beyonce akiimba alimwambia hadhani kama kuimba ni kipaji chake lakini leo hii Beyonce ni miongoni mwa waimbaji wakubwa duniani akiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekani Milioni 600 na kuuza zaidi ya rekodi milioni 34. 2: Shakira . Shakira ni miongoni mwa waimbaji wenye mafanikio makubwa dunia akiwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 220 na kuuza rekodi  zaidi ya milioni 60 duniani kote lakini aliwahi kukataliwa kujiunga na kikundi cha kuimba kwaya kanisani na mwalimu wake wa muziki kumwambia ana sauti mbaya inayofanana na mbuzi. 3

Mfahamu Millard Ayo.

Huyu ndiye @ millardayo . com Mtangazaji wa Radio na Televisheni unayemtazama na kumsikiliza kila siku. Kwa Majina anaitwa Millard Afrael Ayo alizaliwa mkoanni Arusha January 26 akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye famili ya watoto wanne ya Afrael Ayo ambae ni mmeru wa Akheri Tengeru, ni mfanyabiashara na mama Mary Ayo ni mwalimu. Baada ya mama yake mzazi kuona uharaka wa uelewa wa Millard, alimuanzisha shule akiwa mdogo sana na hatimae kumaliza elimu ya msingi akiwa na miaka 12 tu, akamaliza form four akiwa na miaka 16 mwaka 2002, sehemu zote hizo yeye ndio alikua mdogo kuliko wote darasani kuanzia Patandi Primary School Tengeru, Akeri Secondary School na Mbezi Beach High School. Wakati akisubiri majibu, Millard alijiunga na Arusha College of Electronics na kusomea ufundi wa kutengeneza satelitte dish, tv deck na radio masomo ambayo aliyamaliza na aliyasoma kwa sababu ilikua ni kazi ya pili aliyoipenda, baada ya hapo mama yake mzazi alishawishiwa na marafiki zake ili Millard

Manyanyaso kwa mtoto husababisha kuwahi Kubarehe Mapema.

DUNIANI UTAFITI: Manyanyaso kwa mtoto husababisha kubalehe mapema. Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Penn State, Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa zaidi ya 90% ya watoto waliopitia maisha ya kunyanyaswa, kupigwa au kudhalilishwa kingono wanabalehe haraka ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo. Professor Jennie Noll aliliambia Jarida la Adolescent Health: >>> “Watoto hasa wa kike wanaolelewa kwa kunyanyawa hasa kupigwa au kubakwa hubalehe kabla ya muda ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo pia watoto wa aina hii huota matiti mapema ukilinganisha na watoto wa kawaida.“ Akielezea uhusiano ulipo baina ya mtoto kunyanyaswa na kubalehe kabla ya wakati Dr. Noll alisema watoto wanaokuwa katika mazingira kama hayo huzalisha homoni nyingi zinazotokana na msongo mkubwa wa mawazo hivyo kuharakisha muda wa balehe. Wanasaikolojia hao pia walisema mtoto anayenyanyaswa yuko hatarini zaidi kupata saratani ya ovari na matiti ukilinganisha na watoto a

Nusu ya Wamarekani wahitaji Donald Trump aondelewe.

DUNIANI Nusu ya Wamarekani wataka Donald Trump aondolewe madarakani. Taasisi ya utafiti ya sera za umma Marekani imetoa matokeo ya utafiti uliofanywa February 2017 kuhusu utendaji kazi wa Rais wa nchi hiyo ambapo  zaidi ya nusu ya Wananchi wameonesha kumkataa Donald Trump huku zaidi ya asilimia 44 wakilitaka Bunge la nchi hiyo kupiga kura za kumuondoa madarakani. Kwa mujibu wa utafiti huo asilimia 44 ya watu wamejutia kumchagua Donald Trump baada ya kufuta sera ya afya iliyoanzishwa na Rais Obama “Obamacare” bila kuweka sera mpya huku asilimia 44 walisema ni mtu asiye muaminifu na asilimia 64 wakimtaka Rais huyo kuonesha hadharani mlolongo wake wa ulipaji kodi. Utafiti huo pia umeonesha Donald Trump anashika namba tatu kati ya wanasiasa wanaochukiwa na wananchi kwa sasa huku akiongozwa na Msemaji Mkuu wa Bunge Paul Ryan.

Taarifa Kuhusu Mgomo wa Mabasi.

Taarifa kuhusu mgomo wa mabasi kesho. Mgomo wa usafirishaji wa abiria na mizigo usio na kikomo uliopangwa kufanyika kuanzia kesho April 4 2017 na chama cha wamiliki wa mabasi na malori nchini sasa umesitishwa, mgomo huo ulikuwa unapinga sheria zilizotungwa na Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini ‘SUMATRA’ ambazo zinatajwa kuwa na vifungu amabvyo ni kandamizi vinavyoweza kutishia ustawi biashara ya mabasi nchini. Mgomo huo umesitishwa baada ya wamiliki hao kukutana na Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na SUMATRA na kufikia makubaliano kwa yale ambayo walikuwa wameyataka yafanyiwe marekebisho.

Nchi 21 Duniani ambazo Raia wake siyo Walarimu.

Nchi 21 Duniani ambazo Raia wake siyo wakarimu, Afrika imetajwa nchi moja tu. # millardayo. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Wroclaw Poland wametoa list ya nchi zenye wananchi wasiokuwa wakarimu duniani ambapo Romania imeshika namba moja ikifuatiwa na Hungary ambapo kwa mujibu wa utafiti huo watu wa Romania wanaongoza duniani kwa kuchukia ukaribu na mtu, kwa wastani mtu hutaka usimame sentimita 139 kutoka alipo. Katika list hii nchi pekee kutoka Afrika ni Uganda ambapo imeshika namba tano kwa kuwa na watu wasiowakarimu duniani, huku mtu akitaka usisimame karibu yake kwa sentimita 127. Tazama list ya nchi 21 duniani zenye raia wasiowakarimu duniani, stori hii ni kwa mujibu wa www.indy100.com

Wanyama wanaopewa Heshima kubwa za Kijeshi.

DUNIANI Viumbe watano wanaopewa heshima kubwa jeshini mbali na binadamu By Farhiyah Adam. Kwa kawaida wanyama hurahisisha maisha ya binadamu kwa kuwa walinzi, chakula na usafiri, lakini kuna baadhi ya wanyama na ndege walioweza kujiwekea heshima duniani hasa  kwenye sekta maalum za kijeshi na wameweza kupata nafasi za juu jeshini. 1: Sir Nils Olav Nils Olav ni ndege aina ya Penguin aliyepewa cheo mara ya kwanza mwaka 1972 na kuwekwa kwenye timu ya walinzi wa mfalme Harald V Loudon wa Norway. Kwa sasa Sir Nils Olav ni Brigedia anapewa heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa saluti na kukagua jeshi. 2: Treo Ni mbwa aliyetumikia jeshi la Uingereza kuanzia mwaka 2001 mpaka 2015. Trio ana medali zisizopungua 63 ambazo alipewa baada ya kufaya kazi kubwa ya kutegua mabomu na kutambua mahali mabomu yalipofichwa. 3: William of Orange. William ni njiwa aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uingereza mwenye namba MI14 ambapo mwaka 1944 alipewa medali ya 21 baada ya kupeleka ujumbe uliookoa v

Dawa ya Kuzuia Kuzeeka kwa Vinasaba(DNA).

DUNIANI UTAFITI: Naambiwa imegundulika dawa ya kuzuia usizeeke na inatibu kisukari. @Tza millardayo. April 2 2017 nimekutana na stori ambayo inawahusu wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha New South Wales Marekani kugundua dawa zitakazomzuia mtu kuzeeka, huku zikisaidia kurekebisha seli za mtu aliyezeeka na kurekebisha vinasaba ‘DNA’ vilivyoharibika ambavyo ndio sababu kuu ya uzee. Mkuu wa utafiti huo Professor David Sinclair aliiambia Science Today kuwa: >>>” Dawa hizi zitazuia uzee kwa kupambana na magonjwa yote yanayosababisha ngozi na mifupa ya binadamu kuharikibika. Itaponya magonjwa kama Kisukari, Saratani na magonjwa mengine yanayosababishwa na uzee, pia itasaidia kulinda kiwango cha mafuta mwilini ‘Calories’ na kuongeza maisha marefu ” Ripoti ya utafiti huo ilionesha jaribio la kwanza lilifanywa kwa panya mzee ambapo baada ya wiki moja kulikuwa na mabadiliko chanya kwenye ngozi na seli zake zikionekana kuimarika kwa kiasi kikubwa, huku jaribio la kwanza kwa binadamu li

Watu Kumi wenye Akili ya Juu(High IQ) Duniani.

DUNIANI Wajue watu kumi wenye akili zaidi duniani By Team @millardayo. Kipimo cha IQ ni njia pekee inayoaminiwa kupima uwezo wa akili za mtu ambapo kwa kawaida binadamu wengi wana IQ ya kuanzia 90 mpaka 110 lakini watu wachache sana wana IQ level ya kuanzia 140 na kuendelea. Leo nimekuletea hii list ya watu kumi wanaoaminikia kuwa na akili hadi kufikia mwaka 2017. 1: Terrence Tao Ni mwanahisabati kutoka Marekani ambaye anakadiriwa kuwa na IQ level ya 230. Terence Tao aliweza kufanya hisabati akiwa na miaka 2 na alipokuwa na miaka 7 aliweza kufanya hesabu ngumu za level ya Chuo Kikuu akiwa na miaka 20 alipata PhD. Mwaka 2006 alishinda medali  ya Field na mwaka 2014 alipata tuzo ya Breakthrough prize in mathematics. 2: Christopher Hirata Ni Mnajimu aliyebobea katika mambo ya anga ambapo kwa sasa anafanya kazi katika Shirika la Mambo ya Anga la Marekani ‘NASA’. Anatajwa kuwa na IQ level ya 225 ambapo akiwa na miaka 13 alipata tuzo ya Mwanahisabati Bora wa Dunia  na kuweza kupata PhD

Darassa-Too Much.

Listen new  Audio from  Darassa known as Too Much. Follow the link below to listen and downloading it. http:// bekaboy.com /2016/07/ darassa-much / Thanks for visiting www . dbmclassic . blogspot . com /

Ubungo Flying Over how it will look like.

Ubungo Flying Over Roads.how it will looks like follow the link below to watch and downloading it: https://youtu.be/FZ5x2QGpFYk

Darassa-Utanitoa Roho.

Download and Listen new Audio from Tanzania Hip Hop Rapper known as Darassa the song is known as Utanitoa Roho. Darassa- Utanitoa Roho Official Audio.: https :// youtu.be / bJALNnhavbQ Thanks foe visiting www . dbmclassic . blogspot . com /