Viwanja Kumi Bora Afrika,Ukanda wa Mashariki Upo mmoja tu.

TOP 10 ya viwanja ghali zaidi Afrika, Afrika Mashariki upo mmoja.

Licha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF kusema moja ya sababu kuu inayopelekea Bara la Africa kufanya vibaya kwenye mchezo wa mpira wa miguu duniani ni ukosefu wa viwanja bora, kuna baadhi ya nchi Afrika zina viwanja vizuri na vyenye gharama kubwa ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea.

Leo April 10, 2017 nimekuletea list ya viwanja 10 vizuri na vyenye gharama zaidi barani Afrika hadi kufikia December 2016.

1: Capetown Stadium, Afrika Kusini

Uwanja huu una uwezo wa kuingiza mashabiki 64,100 ambapo umejengwa na kampuni ya Afrika Kusini ukiigharimu nchi hiyo Dollar 600 million ukiwa ndiyo uwanja wenye gharama kwa Afrika.

2: Moses Madiba Stadium, Afrika Kusini

Moses Madiba ulikuwa moja ya viwanja vilivyotumika wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2010 ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 62,760. Uligharimu Dollar 450 million.

3: FNB Stadium, Afrika Kusini

Uwanja huu unashikilia rekodi ya kuwa uwanja mkubwa zaidi Africa ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 94,736. FNB Stadium ulitumika kwa michezo mingi wakatai wa Fainali za Kombe la Dunia 2010 na kina gharama ya Dollar 440 million.

4: Abuja Stadium, Nigeria

Huu ndiyo uwanja mkubwa zaidi Nigeria. Abuja Stadium una uwezo wa kuingiza mashabiki 60,491 ukiwa na thamani ya Dollar 360 million.

5: Nelson Mandela bay Stadium, Afrika Kusini

Uwanja huu unapatikana Port Elizabeth, Afrika Kusini ambapo ulipewa jina la Rais wa kwanza mwesui wa nchi hiyo, Nelson Mandela ambapo una uwezo wa kuingiza mashabiki 48,459 ukiwa na thamani ya Dollar 270 million.

6: November 11 Stadium, Angola

Uwanja huu upo katika mji mkuu wa Angola, Angola na umepewa jina la Siku ya Uhuru wa nchi hiyo. Uwanja huu unaweza kuingiza zaidi ya mashabiki 50,000 ukiwa ni moja ya viwanja vilivyotumika kwenye AFCON 2010. Gharama yake ni Dollar 227 million.

7: Peter Mokaba Stadium, Afrika Kusini

Ni miongoni mwa viwanja vilivyojengwa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini. Peter Mokaba Stadium una uwezo wa kuingiza mashabiki 41,733 ukiwa na gharama ya zaidi Dollar 150 million.

8: Mbombela Stadium, Afrika Kusini

Huu ndio uwanja mdogo zaidi kati ya viwanja vilivyojengwa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia 20101 nchini Afrika Kusini. Uwanja huu una viti 40,929 ukiwa ndio uwanja pekee uliojengwa kwa kodi za wananchi ambapo uligharimu Dollar 140 million.

9: Stade Olimpique de Rades, Tunisia

Uwanja huu upo nchini Tunisia na unaweza kuingiza mashabiki 60,000 ukiwa umejengwa kwa zaidi ya Dollar 110 million.

10: Benjamin Mkapa Stadium, Tanzania

Uwanja pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ambao ulijengwa mwaka 2005 na aliyekuwa Rais wa Tatu wa Tanzania Benjamin William Mkapa. Uwanja huu uliigharimu serikali ya Tanzania Dollar 53 million ambapo una uwezo wa kuingiza zaidi ya mashabiki 60,000.

Comments

Popular posts from this blog

Taarifa Kuhusu Kupotea Kwa Msanii Roma Mkatoliki.

Taarifa Kuhusu Mgomo wa Mabasi.