Taarifa Kuhusu Kupotea Kwa Msanii Roma Mkatoliki.
Taarifa zilizopo ni kuwa Msanii Roma Mkatoliki kutokea katika Studio ya Tongwe (Tongwe Rocords) alivamiwa na watu wasiojulikana Majira ya Usiku wa kuamkia Siku ya Alhamisi.
Msanii huyo alivamiwa Studioni hapo akiwa studioni hapo na kupelekwa sehemu kusilojulikana pamoja na mwemzake Moni au @centralzone kama anavyojulikana.
Familia ya Msanii Roma (Mkewe) ameweza kusema kuwa simu ya Msanii huyo(Mmewe) imekuwa ikiita tu bila kupokelewa hivyo akiwaomba Watanzania wote waweze kumpa ushirikiano wa taarifa zozote za kuhusiana na Msanii Roma (Mmewe) sehemu yoyote ile ambapo zlatapatikana.
Comments