Wanasayansi wamegundua Tiba ya Hangover.
Utafiti Mpya kutoka kwa Wanasayansi, wamegundua tiba ya Hangover
Hii ni dunia ambayo kila siku watu wanafanya utafiti wa mambo mbaimbali…sasa leo April 7, 2017 nakuletea matokeo ya utafiti uliofanywa na wanafunzi wa wawili nchini Marekani waliogundua tiba ya hangover.
Unaambiwa katika stori iliyochapishwa na Daily Mail March 29, 2017, wanafunzi wawili kutoka Yale University wamegundua tiba hiyo ambayo wameapa jina la SunUp ikiwa ni unga uliotokana na mchanganyiko wa viungo vya asili ambao umegunduliwa kwa lengo la kuvunja vunja molikuli za sumu kwenye ini, na kubalansi glutamine pamoja na kuuamsha mwili kwa elektroliti baada ya kunywa pombe.
Margaret Morese na Liam McClintock ambao waliathiwa sana na Hangover waligundua tiba hiyo baada ya kujaribu viungo vya asili kila kimoja kivyake katika tafiti huru kuthibitisha uwezo wake dhidi ya kuondoa athari za kilevi na ulinzi thabiti dhidi ya sumu itokanayo na kilevi kwa mtumiaji na baadaye kutengeneza unga huo ambao humtaka mtumiaji kuuchanganya kwenye maji na kunywa kabla ya kutumia kilevi.
“Pamoja kwa msaada wenu tunakusudia kuzikinga athari za uharibifu wa kilevi kwenye mwili, hisia mbaya za hangover, na nguvukazi zinazopotea kutokana na kilevi.” –Liam McClintock.
Comments