Wanyama wanaopewa Heshima kubwa za Kijeshi.

DUNIANI Viumbe watano wanaopewa heshima kubwa jeshini mbali na binadamu
By Farhiyah Adam.

Kwa kawaida wanyama hurahisisha maisha ya binadamu kwa kuwa walinzi, chakula na usafiri, lakini kuna baadhi ya wanyama na ndege walioweza kujiwekea heshima duniani hasa  kwenye sekta maalum za kijeshi na wameweza kupata nafasi za juu jeshini.

1: Sir Nils Olav

Nils Olav ni ndege aina ya Penguin aliyepewa cheo mara ya kwanza mwaka 1972 na kuwekwa kwenye timu ya walinzi wa mfalme Harald V Loudon wa Norway. Kwa sasa Sir Nils Olav ni Brigedia anapewa heshima zote za kijeshi ikiwemo kupigiwa saluti na kukagua jeshi.

2: Treo

Ni mbwa aliyetumikia jeshi la Uingereza kuanzia mwaka 2001 mpaka 2015. Trio ana medali zisizopungua 63 ambazo alipewa baada ya kufaya kazi kubwa ya kutegua mabomu na kutambua mahali mabomu yalipofichwa.

3: William of Orange.

William ni njiwa aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la Uingereza mwenye namba MI14 ambapo mwaka 1944 alipewa medali ya 21 baada ya kupeleka ujumbe uliookoa vifo vya zaidi ya wanajeshi 2000 kwenye vita ya Arnhem wakati wa Vita ya Pili ya Dunia.

4: Taffy IV.

Huyu ni mbuzi aliyetumikia jeshi la Uingereza tangu mwaka 1775 ambaye alichukuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1774 na kuingizwa kwenye jeshi maalum la Uingereza alipokutwa anarandaranda porini. Alipewa medali ya 14 ambayo ni maalum waliyopewa wanajeshi wa Uingereza wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia (WWI).

5: LIN WANG

Ni tembo aliyekuwa mwanajeshi wa jeshi la China kuanzia mwaka 1942 ambapo alitumika kujenga majengo marefu ya jeshini, kusafirisha chakula wakati wa vita na alitumika kama kivutio kwa ajili ya kukusanya fedha wakati wa njaa kipindi cha vita na kupewa medali 12 za kijeshi.

Comments

Popular posts from this blog

Taarifa Kuhusu Kupotea Kwa Msanii Roma Mkatoliki.

Taarifa Kuhusu Mgomo wa Mabasi.