Viwanja Kumi Bora Afrika,Ukanda wa Mashariki Upo mmoja tu.
TOP 10 ya viwanja ghali zaidi Afrika , Afrika Mashariki upo mmoja . Licha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF kusema moja ya sababu kuu inayopelekea Bara la Africa kufanya vibaya kwenye mchezo wa mpira wa miguu duniani ni ukosefu wa viwanja bora, kuna baadhi ya nchi Afrika zina viwanja vizuri na vyenye gharama kubwa ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea. Leo April 10, 2017 nimekuletea list ya viwanja 10 vizuri na vyenye gharama zaidi barani Afrika hadi kufikia December 2016. 1: Capetown Stadium, Afrika Kusini Uwanja huu una uwezo wa kuingiza mashabiki 64,100 ambapo umejengwa na kampuni ya Afrika Kusini ukiigharimu nchi hiyo Dollar 600 million ukiwa ndiyo uwanja wenye gharama kwa Afrika. 2: Moses Madiba Stadium, Afrika Kusini Moses Madiba ulikuwa moja ya viwanja vilivyotumika wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2010 ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 62,760. Uligharimu Dollar 450 million. 3: FNB Stadium, Afrika Kusini Uwanja huu unashikilia rekodi ya...