Walicholisema Stamina na Bill Bass kuhusiana na utekaji huku wakiitambulisha Ngoma Yao Mpya.

Stamina na Bill Nass wamezungumzia kuhusu utekaji.

Leo April 12 2017 kupitia kwenye XXL ya Clouds FM wakali kutoka Bongoflevani Bill Nass na Stamina wamezungumzia kuhusu vitendo vya utekaji watu baada ya Roma Mkatoliki na wenzake watatu kutekwa na watu wasiojulikana kabla ya kuonekana.

Stamina amedai kuwa haoni sababu nyingine zaidi ya muziki ambao umekuwa hukisababisha utekaji hivyo kuwanyima uhuru wa sanaa, huku Bill Nass akisema hatumii muda mwingi kutoka nje kabla na  baada ya saa sita usiku kuhofia kutekwa.

>>>“Sioni kama kuna kitu kingine zaidi ya muziki. Ndiyo sababu nayaona matukio ya utekaji kama ni kutunyima uhuru wa sanaa yetu."
-Stamina.

>>>”Siku hizi situmii muda mwingi nje. Watu wangu wa karibu wanapenda niwepo ndani kabla ya saa sita usiku juu ya hofu ya utekaji.
-Billnass.

Bill Nass na Stamina wamezitoa kauli hizo wakati wakiutambulisha wimbo wao mpya unaoitwa Aje mwenyewe walioshirikiana wasanii watatu ambao ni Stamina, Young Killer na Bill Nass wakisema wimbo huo unatokana na wazo la Young Killer kuwaunganisha.

>>>Asilimia 80 ya Shout out ya hii ngoma iende kwa Young Killer ndiye aliyetuunganisha kufanya kazi kwa pamoja.”
-Stamina.

>>>Hii ngoma tulihitaji awepo msanii mwingine wa kike, lakini alikosekana. Sijafahamu ni kwa nini, lakini hii ni ngoma ya wote.”
-Young Killer.

Comments

Popular posts from this blog

Taarifa Kuhusu Kupotea Kwa Msanii Roma Mkatoliki.

Taarifa Kuhusu Mgomo wa Mabasi.