Watu Kumi wenye Akili ya Juu(High IQ) Duniani.
DUNIANI Wajue watu kumi wenye akili zaidi duniani By Team @millardayo. Kipimo cha IQ ni njia pekee inayoaminiwa kupima uwezo wa akili za mtu ambapo kwa kawaida binadamu wengi wana IQ ya kuanzia 90 mpaka 110 lakini watu wachache sana wana IQ level ya kuanzia 140 na kuendelea. Leo nimekuletea hii list ya watu kumi wanaoaminikia kuwa na akili hadi kufikia mwaka 2017. 1: Terrence Tao Ni mwanahisabati kutoka Marekani ambaye anakadiriwa kuwa na IQ level ya 230. Terence Tao aliweza kufanya hisabati akiwa na miaka 2 na alipokuwa na miaka 7 aliweza kufanya hesabu ngumu za level ya Chuo Kikuu akiwa na miaka 20 alipata PhD. Mwaka 2006 alishinda medali ya Field na mwaka 2014 alipata tuzo ya Breakthrough prize in mathematics. 2: Christopher Hirata Ni Mnajimu aliyebobea katika mambo ya anga ambapo kwa sasa anafanya kazi katika Shirika la Mambo ya Anga la Marekani ‘NASA’. Anatajwa kuwa na IQ level ya 225 ambapo akiwa na miaka 13 alipata tuzo ya Mwanahisabati Bora wa Dunia ...