Kufikia 2018 haya ndiyo maamuzi watakayofikia Canada kuhusu Bangi. Kadiri siku zinavyobadilika na miaka kusonga mbele ndivyo nchi mbalimbali duniani hufanya marekebisho katika sheria za nchi kulingana na hitajio la wananchi kwa maendeleo ya Taifa. Leo April 14, 2017 mtandao maarufu wa CNN umeripoti taarifa kuhusu mpango wa Serikali ya Canada chini ya Waziri Mkuu Justin Trudeau kuweka wazi mipango yake ya kuhalalisha bangi ifikapo 2018 ambapo kama Bunge la nchi hiyo litapitisha muswada huo, Canada itakuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kuhalalisha soko la bangi. Waziri Mkuu aliandika kwenye account yake ya Twitter: “ Ni rahisi sana kwa watoto wetu kupata bangi. Tutaibadilisha.“ – Justin Trudeau . Licha ya kutaka kuhalalisha bangi, pia yametajwa mambo matano ya kuyafahamu kuhusu pendekezo la Canada katika sera ya bangi ambayo rasmi itakuwa July 2018. 1: Serikali kusimamia mauzo ya bangi Serikali ya Canada itaweka mfumo maalum wa kuzalisha, kusambaza ...
Comments