Posts

Showing posts from April 11, 2017

RFEF Imemfungia Neymar Mechi tatu mfululizo.

BAD NEWS: RFEF imemfungia Neymar leo April 11 2017. Staa wa soka wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Neymar amekutana na adhabu ya kufungiwa mechi 3 mfululizo  kuichezea FC Barcelona na shirikisho la soka Hispania ( Royal Spanish Football Federation (RFEF) kwa makosa mawili. Neymar amefungiwa mechi tatu, mechi moja ni kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano wakati wa mchezo dhidi ya Malaga uliyomalizika kwa FC Barcelona kupoteza kwa magoli mawili kwa 2-0 lakini mechi ya mbili kwa kosa la kumpongeza kwa kejeli fourth official wakati anatoka nje ya uwanja. Neymar alipooneshwa kadi ya pili ya njano, Mchezaji huyo raia wa Brazil alitoa lugha za kejeli kwa fourth official wakati anatoka uwanjani kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano, refa wa game hiyo Jesus Gil Manzano ndio aliandika ripoti hiyo, Neymar sasa atakosa mchezo dhidi ya Real Sociedad, Real Madrid na Osasuna.

Wajumbe Walioapishwa na Mheshimiwa Raisi ili kwenda kufanya Uchunguzi wa Makontena yaliotoka nchini Tangu Mwaka 1998.

Rais Maghufuli amewaapisha Wajumbe wa Kamati Maalumu . Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo April 11, 2017 amewaapisha Wajumbe wa Kamati Maalum ya pili ya wachumi na wanasheria ambayo itachunguza mchanga wenye madini uliomo kwenye makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini. Wajumbe walioapishwa ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Nehemiah Eliachim Osoro na wajumbe wake ambao ni Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara, Dkt. Oswald Joseph Mashindano, Bw. Casmir Sumba Kyuki, Bw. Andrew Wilson Massawe na Bw. Gabriel Pascal Malata . Wengine ni Bw. Usaje Bernard Usubisye na Bi. Butamo Kasuka Philip ambapo baada ya kuwaapisha wajumbe hao Rais Magufuli amesema ameunda kamati hiyo ili ifanye uchunguzi wa kina utakaobaini aina ya madini yaliyomo ndani ya mchanga huo, thamani yake, kiwango cha kila aina ya madini, uzito wa mchanga unaowekwa ndani ya makontena na kujua ni makontena mangapi yamepitishwa tangu mwaka 1998. “ Kafuatilieni makontena mangapi yametoka hapa nchini na kupe...

Sifa za wanaotakiwa kujiunga na Mafunzo ya Afya Ngazi ya Cheti na Stashahada(Diploma).

Kwa wale wanaohitaji kutumq mombi kwa ajili ya mafunzo ingia link hii hapa chini ili kuweza kutazama Sifa za waombaji mafunzo ya Afya katika Ngazi za Cheti na Stashahada yaani Diploma. http:// maswayetu.blogspot.nl /2017/04/ taarifa-muhimu-kuhusu-sifa-za-kujiunga.html .