Stori Kumi za Uharifu Zitakazokushangaza Zaidi.
Stori Kumi(10) za wahalifu zitakazokushangaza duniani.
Wahalifu wengi hutumia akili nyingi wakati wa kufanya uhalifu ili wasikamatwe au kutiwa nguvuni na vyombo vya dola lakini mara nyingine hujikuta wamefanya makosa madogo madogo ambayo huwakamatisha na kujikuta mikononi mwa sheria.
1: Joseph Martin
Joseph Martin kutokea Florida Marekani alipiga simu Polisi kushitaki baada ya kuagiza bangi na muuzaji kukimbia na pesa yake. Badala ya Polisi kumsaidia shida yake walimtafuta na kumkamata kwa kosa la kutumia mihadarati ambayo imezuiwa kisheria.
2: Tyron Jr
Tyron Jr kutokea Carlifornia Marekani alikwenda Mahakamani kusikiliza kesi yake ya wizi wa gari lakini alijikuta akipata kesi mbili baada ya Polisi kugundua gari aina ya Lexus SUV alilokuja nalo Mahakamani hapo aliliiba miezi michache iliyopita kabla ya kukamatwa kwa kesi ya pili.
3: Jonathan Parker
Jonathan Parker alivamia nyumba moja katika mji wa Pennsylvania Marekani ambapo baada ya kuiba vitu kadhaa aliamua kuingia kwenye mtandao wa Facebook kwa kutumia computer ya nyumba hiyo na kusahau ku-log out hivyo kuwarahisishia Polisi kutumia account yake kupata picha zake na kumkamata.
4: Krystian Bala
Krystian Bala aliona fursa kwenye uandishi wa vitabu na kuamua kuandika stori inayohusu mauaji aliyoyafanya zaidi ya miaka kumi nyuma ambapo baada ya Polisi kusoma kitabu hiki waligundua stori hii inafanana na kesi ya mauaji ambayo hakupatikana mtuhumiwa hivyo Polisi walimkamata Krystian Bala mara moja na kumshitaki.
5: Quinton Thomas
Akiwa mahabusu kwa kosa la unyang’anyi, Quinton Thomas alimuandikia barua rafiki yake awaue mashahidi wote wa kesi yake ya wizi lakini alikosea anuani ya rafiki yake huyo na barua kurudishwa na Polisi kuisoma, Alishtakiwa kwa makosa mengine matatu ya kujaribu kuua.
6: Marque Moore
Marque Moore kutoka Richmond, California alijikuta mikononi mwa Polisi baada ya kuiba baiskeli na kuumuuzia mtu aliyemuibia bila kujua.
7: Mark Smith
Mark Smith kutoka Uingereza aliandikwa kama mhalifu mjinga sana duniani baada ya kuingia katika nyumba ya Stephene Marks kwa lengo la kuiba lakini alishindwa kutekeleza azma yake hiyo baada ya kupitiwa na usingizi na kulala chini ya kitanda hadi Polisi walipomkamata.
8: Ruben Zarate
Mwaka 2008 Ruben Zarate alivamia duka moja mjini Chicago kwa lengo la kuiba lakini alipokuta pesa zimefungiwa kwenye droo na Manager hakuwepo aliamua kumpa namba za simu msaidizi wake ili akirudi apigiwe simu aje kuiba lakini aliishia Polisi.
9: Klaus Schmidt
Mwaka 1995 Klaus Schmidt alivamia Bank mjini Berlin, Ujerumani lakini wafanyakazi wa Bank hiyo waligundua ni kiziwi na kuamua kupiga alarm ambayo Klaus Schmidt alikuwa haiskii ambapo dakika chache baadaye Polisi walifika na kumkamata.
10: Albert Bailey
Mwaka 2010 Albert Bailey alitaka kuvamia Bank na kuamua kupiga simu kuwataarifu wafanyakazi wa Bank watayarishe fedha kwani atakuja kuvamia Bank hiyo saa chache zijayo lakini alijikuta mikononi mwa Polisi.
Comments