Maamuzi ya Canada Kuhusu Bangi Itakapofikia 2018 Ni haya.

Kufikia 2018 haya ndiyo maamuzi watakayofikia Canada kuhusu Bangi.

Kadiri siku zinavyobadilika na miaka kusonga mbele ndivyo nchi mbalimbali duniani hufanya marekebisho katika sheria za nchi kulingana na hitajio la wananchi kwa maendeleo ya Taifa.

Leo April 14, 2017 mtandao maarufu wa CNN umeripoti taarifa kuhusu mpango wa Serikali ya Canada chini ya Waziri Mkuu Justin Trudeau kuweka wazi mipango yake ya kuhalalisha bangi ifikapo 2018 ambapo kama Bunge la nchi hiyo litapitisha muswada huo, Canada itakuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kuhalalisha soko la bangi.

Waziri Mkuu aliandika kwenye account yake ya Twitter: “Ni rahisi sana kwa watoto wetu kupata bangi. Tutaibadilisha.“Justin Trudeau.

Licha ya kutaka kuhalalisha bangi, pia yametajwa mambo matano ya kuyafahamu kuhusu pendekezo la Canada katika sera ya bangi ambayo rasmi itakuwa July 2018.

1: Serikali kusimamia mauzo ya bangi

Serikali ya Canada itaweka mfumo maalum wa kuzalisha, kusambaza na kuuza bangi ambapo itatoza ada na kodi kwa watakaoidhinishwa kuuza bangi wakisema kuwa ni kuchukua faida inayodhibitiwa sasa na wahalifu.

2: Watu wazima wanaweza kuwa na bangi na hata kulima

Watu wazima wataweza kuwa na bangi hadi gramu 30 wawapo hadharani na wataruhusiwa kulima hadi miche minne kwa kila nyumba.

3: Watoto na vijana hawatoruhusiwa kuwa na bangi

Vijana na watoto chini ya umri wa miaka 18, hawatoruhusiwa kumiliki au kununua bangi ambapo sera mpya itatunga sheria kali kwa kuuza bangi kwa mtu wa umri wa chini ya miaka 18 ikipendekezwa miaka 14 jela kwa atakayekutwa na kosa hilo.

4: Hautoruhusiwa kuendesha wakati umevuta bangi

Muswada unaweza kuongeza katazo kwa watu kutoendesha wakati wakiwa wamelewa au kuvuta bangi na dawa nyingine zilizokatazwa.

5: Hautakiwi kuifikisha nje ya mipaka ya nchi

Kuitoa bangi nje ya mipaka kutaweza kuwa kesi kubwa sana – ukizingatia sheria za bangi hutofautiana kulingana na nchi.

Comments

Popular posts from this blog

Taarifa Kuhusu Kupotea Kwa Msanii Roma Mkatoliki.

Taarifa Kuhusu Mgomo wa Mabasi.