Posts

Showing posts from April 21, 2017

Huyu Ndiye Mtoto Mtanzania Anayeaemekana Kuwa na Uelewa na Ujuzi wa Hali ya Juu.

# Ithan #Mahafudh , ni mtoto mwenye umri wa miaka mitatu, ameendelea kuthibitisha #kipaji kikubwa alichonacho, akiwa na uwezo wa kuwataja karibu marais wa nchi zote duniani ambapo #Pasaka hii, alikuwa kivutio kwenye #event iliyoandaliwa na #Shilawadu ambapo alijibu maswali yote ya papo kwa hapo. Mtoto huyo, licha ya uwezo wake wa kutaja majina ya viongozi mbalimbali, anao uwezo mkubwa wa kukariri mambo mengi kwa wakati mmoja. Mtazame zaidi hapa...         http:// bit.ly /2oOwCko Maajabu mengine ya mtoto Ithan ni kuwa anafahamu kuendesha gari na pia anajua kutumia kompyuta na simu za kisasa yaani smartphones, kwani anao uwezo wa kuingia katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Serikali Yawapandisha Watumishi 2000 Vyeo

Watumishi 2,000 Elimu wapandishwa V yeo WAZIRI WA ELIMU, PROFESA JOYCE NDALICHAKO . BUNGE limeelezwa kuwa Jumla ya watumishi 2,272 walipandishwa vyeo katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi katika kipindi cha 2015/16 huku miongoni mwao 71 walitoka Chuo cha Ualimu Korogwe. Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini, Mary Chatanda (CCM), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwapandisha daraja wale waliostahili na kuwa lini itawalipa madai yao ya fedha za likizo ambazo watumishi hawajalipwa kwa muda mrefu na wamekuwa wakishindwa kuzipata kwa wakati. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri huyo alibainisha serikali inaendelea kulipa madeni, ikiwamo fedha za likizo kwa walimu au watumishi katika sekta ya Elimu, ambapo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi Juni 2016, jumla ya Sh. Bilioni  22.7 zililipwa kwa walimu 63,814. Aidha, alisema katika kipindi cha mwaka 2016/...

Machache Kuhusu Korea Kaskazini(North Korea).

MACHACHE ZAIDI KUHUSU KOREA KASKAZINI . 1. Bangi ni Halali kabisa nchi nzima, na haichukuliwi kama ni kitu cha kulewesha yaani Drug. 2. Ndio nchi pekee duniani hadi sasa ambayo imewahi kuiteka meli ya kivita ya wamarekani. 3. Wakati dunia nzima leo ni 2017 kwao ni mwaka 106 wakihesabu kuanzia kifo cha kiongozi wao Kim il-Sung-.Baba wa taifa lao Kim II-Sung alizaliwa 15.04.1912 siku ilipozama meli ya Titanic . (Rais wa Maisha wa Korea Kaskazini ni Kim Il Sung. Mtoto wake na mjukuu wake wamekuja kuwa viongozi tu, lakini yeye mwenyewe babu yao ndiye rais mpaka leo, hata kama amefariki.....Eternal President of the Republic-Hayo ndiyo mambo ya North Korea).    Hiyo siku ndio chanzo cha kalenda yao (Democratic People's Republic of Korea_Juche Korea[/QUOTE] year Gregorian year Dangun year-Kim alizaliwa 1912 ~ hapa ndio juche year inaanzia). 4. Kuanzia 2009 nchi hii sio ya kikomunist tena, wana msimamo au IDEOLOGY yaoo mpya unaitwa " JUCHE " wakimaanisha " KU...