Taarifa Kuhusu Mgomo wa Mabasi.
Taarifa kuhusu mgomo wa mabasi kesho.
Mgomo wa usafirishaji wa abiria na mizigo usio na kikomo uliopangwa kufanyika kuanzia kesho April 4 2017 na chama cha wamiliki wa mabasi na malori nchini sasa umesitishwa, mgomo huo ulikuwa unapinga sheria zilizotungwa na Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini ‘SUMATRA’ ambazo zinatajwa kuwa na vifungu amabvyo ni kandamizi vinavyoweza kutishia ustawi biashara ya mabasi nchini.
Mgomo huo umesitishwa baada ya wamiliki hao kukutana na Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa na SUMATRA na kufikia makubaliano kwa yale ambayo walikuwa wameyataka yafanyiwe marekebisho.
Comments