Posts

Showing posts from April 15, 2017

Aliyoyasema Mwigulu Nchemba Kuhusu Mauwaji ya Askari Nane.

Mwigulu Nchemba baada ya kutembelea eneo walilouawa Askari Nane . Wakati jioni ya April 13 2017 Wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, iliripotiwa kuwa watu wanaosadikika kuwa majambazi ambao haijafahamika idadi yao wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la polisi na kuwaua askari nane na kumjeruhi mmoja Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba   leo April 14 2017 ametembelea eneo lilipotokea tukio la mauaji ya Askari nane wa Jeshi la Polisi na kusema kuwa waliotekeleza mauaji hayo watalipa damu ya akari hao iliyomwagika.

Maamuzi ya Canada Kuhusu Bangi Itakapofikia 2018 Ni haya.

Kufikia 2018 haya ndiyo maamuzi watakayofikia Canada kuhusu Bangi. Kadiri siku zinavyobadilika na miaka kusonga mbele ndivyo nchi mbalimbali duniani hufanya marekebisho katika sheria za nchi kulingana na hitajio la wananchi kwa maendeleo ya Taifa. Leo April 14, 2017 mtandao maarufu wa CNN umeripoti taarifa kuhusu mpango wa Serikali ya Canada chini ya Waziri Mkuu Justin Trudeau kuweka wazi mipango yake ya kuhalalisha bangi ifikapo 2018 ambapo kama Bunge la nchi hiyo litapitisha muswada huo, Canada itakuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kuhalalisha soko la bangi. Waziri Mkuu aliandika kwenye account yake ya Twitter: “ Ni rahisi sana kwa watoto wetu kupata bangi. Tutaibadilisha.“ – Justin Trudeau . Licha ya kutaka kuhalalisha bangi, pia yametajwa mambo matano ya kuyafahamu kuhusu pendekezo la Canada katika sera ya bangi ambayo rasmi itakuwa July 2018. 1: Serikali kusimamia mauzo ya bangi Serikali ya Canada itaweka mfumo maalum wa kuzalisha, kusambaza ...

Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Mauwaji ya Askari Nane.

Kauli ya Jeshi la Polisi kuhusu mauaji ya askari polisi nane . Jana April 13 2017 jioni Wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, iliripotiwa kuwa watu wanaosadikika kuwa majambazi ambao haijafahamika idadi yao wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la polisi na kuwaua askari nane na kumjeruhi mmoja. Leo April 14 2017 katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo , Nsato Marijani amesema katika tukio hilo majambazi hao walipora silaha saba ; SMG nne na Lon Range tatu. Aidha, Marijani amesema mara baada ya tukio hilo, hatua za kiintelijensia na kipelelezi ambazo zilichukuliwa askari kufuatilia, zilibaini maficho ya muda ya majambazi hao ambapo katika majibizano ya risasi majambazi wanne waliuawa na bunduki nne kupatikana hivyo amesema kuanzia sasa Jeshi la Polisi linakwenda kwenye oparesheni maalumu kupambana na majambazi hao.