Alichokiandika Mbunge Hessein Bashe kuhusu Roma Mkatoliki.
Alichokiandika Mbunge Hussein Bashe kuhusu Roma Mkatoliki By Rama Mwelondo . TZA . Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatoliki zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuripotiwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa Studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana. Watu mbalimbali ikiwemo wasanii mbalimbali wamekuwa wakionesha hisia zao juu ya tukio hilo kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuoneshwa kuguswa na tukio hilo, Mbunge wa Nzega Hussein Bashe ni miongoni mwa watu waliyotumia kuraza zao za instagram kuandika anachowaza kuhusu Roma. Who is behind all this? “ Ni genge ambalo limejipa mamlaka ya kupandikiza woga na chuki miongoni mwa jamii na kuharibu Taswira ya CCM. Tunawajibu wa kukataa woga ,Tunawajibu wa kutoruhusu Misuse ya vyombo vya Ulinzi na usalama, Tunawajibu wa kulinda Taifa letu ” “ Tunawajibu wa kupigania Values zilizopiganiwa na waasisi wa Tai...