Walicholisema Stamina na Bill Bass kuhusiana na utekaji huku wakiitambulisha Ngoma Yao Mpya.
Stamina na Bill Nass wamezungumzia kuhusu utekaji . Leo April 12 2017 kupitia kwenye XXL ya Clouds FM wakali kutoka Bongoflevani Bill Nass na Stamina wamezungumzia kuhusu vitendo vya utekaji watu baada ya Roma Mkatoliki na wenzake watatu kutekwa na watu wasiojulikana kabla ya kuonekana. Stamina amedai kuwa haoni sababu nyingine zaidi ya muziki ambao umekuwa hukisababisha utekaji hivyo kuwanyima uhuru wa sanaa, huku Bill Nass akisema hatumii muda mwingi kutoka nje kabla na baada ya saa sita usiku kuhofia kutekwa. >>>“ Sioni kama kuna kitu kingine zaidi ya muziki. Ndiyo sababu nayaona matukio ya utekaji kama ni kutunyima uhuru wa sanaa yetu ." - Stamina . >>>” Siku hizi situmii muda mwingi nje. Watu wangu wa karibu wanapenda niwepo ndani kabla ya saa sita usiku juu ya hofu ya utekaji. ” - Billnass . Bill Nass na Stamina wamezitoa kauli hizo wakati wakiutambulisha wimbo wao mpya unaoitwa Aje mwenyewe walioshirikiana wasa...