Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Mauwaji ya Askari Nane.
Kauli ya Jeshi la Polisi kuhusu mauaji ya askari polisi nane.
Jana April 13 2017 jioni Wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, iliripotiwa kuwa watu wanaosadikika kuwa majambazi ambao haijafahamika idadi yao wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la polisi na kuwaua askari nane na kumjeruhi mmoja.
Leo April 14 2017 katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Nsato Marijani amesema katika tukio hilo majambazi hao walipora silaha saba; SMG nne na Lon Range tatu.
Aidha, Marijani amesema mara baada ya tukio hilo, hatua za kiintelijensia na kipelelezi ambazo zilichukuliwa askari kufuatilia, zilibaini maficho ya muda ya majambazi hao ambapo katika majibizano ya risasi majambazi wanne waliuawa na bunduki nne kupatikana hivyo amesema kuanzia sasa Jeshi la Polisi linakwenda kwenye oparesheni maalumu kupambana na majambazi hao.
Comments