The Siti Msanii kutoka TONGWE alivyoshuhudia kuchukuliwa kwa Roma.

Shuhuda ameeleza Roma na wenzake walivyochukuliwa Tongwe Records.

Zimepita siku mbili tangu staa wa Hip Hop Bongo Roma kuchukuliwa na watu wasiojulikana pamoja na wenzake wakiwa katika studio za Tongwe Records bila kujulikana walikopelekwa, basi leo April 7, 2017 msanii kutoka Tongwe Records ameelezea jinsi watu hao walivyochukuliwa.

The Siti ameiambia millardayo.com na Ayo TV jinsi Roma Mkatoliki na wenzake walivyochukuliwa Tongwe Records ambapo hadi sasa haijafahamika mahala walipo na watu waliowachukua.

Akizungumza na millardayo.com pamoja na  Ayo TV The Siti alisema:>>>
”Ilitokea kama Jumatano saa kumi na mbili jioni na walikuja watu pale wakashuka kutoka kwenye Noah wakatuambia tuingie ndani ya geti na tukaingia ndani ya geti. Wakamuulizia Junior wakaambiwa hayupo, kisha wakamuulizia na Roma Mkatoliki wakaomba waitiwe Roma kisha walipoitiwa Roma, walimuhoji pale mara wakaingia studio wakachukua vitu na wakawachukua wakina Moni.”
-The Siti.

Comments

Popular posts from this blog

Taarifa Kuhusu Kupotea Kwa Msanii Roma Mkatoliki.

Taarifa Kuhusu Mgomo wa Mabasi.