Manyanyaso kwa mtoto husababisha kuwahi Kubarehe Mapema.

DUNIANI UTAFITI: Manyanyaso kwa mtoto husababisha kubalehe mapema.

Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Penn State, Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa zaidi ya 90% ya watoto waliopitia maisha ya kunyanyaswa, kupigwa au kudhalilishwa kingono wanabalehe haraka ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo.

Professor Jennie Noll aliliambia Jarida la Adolescent Health:
>>> “Watoto hasa wa kike wanaolelewa kwa kunyanyawa hasa kupigwa au kubakwa hubalehe kabla ya muda ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo pia watoto wa aina hii huota matiti mapema ukilinganisha na watoto wa kawaida.“
Akielezea uhusiano ulipo baina ya mtoto kunyanyaswa na kubalehe kabla ya wakati Dr. Noll alisema watoto wanaokuwa katika mazingira kama hayo huzalisha homoni nyingi zinazotokana na msongo mkubwa wa mawazo hivyo kuharakisha muda wa balehe.
Wanasaikolojia hao pia walisema mtoto anayenyanyaswa yuko hatarini zaidi kupata saratani ya ovari na matiti ukilinganisha na watoto ambao hulelewa kwenye mazingira ya upendo na amani.

Comments