Wasanii Waliowahi Kuambiwa hawajui kuimba lakini sasa ni Mastaa.
BURUDANI Waimbaji 10 waliowahi kuambiwa hawajui kuimba lakini leo ni mastaa wa Dunia. Mara nyingi watu wanaposhindwa na jambo hukata tamaa lakini kushindwa mara moja haimaanishi huwezi kufanikiwa jambo hilo ukijaribu tena na tena, leo nimekuletea list ya wanamuziki kumi waliowahi kuambiwa hawajui kuimba na leo hii ni mastaa wakubwa duniani. 1: Beyonce . Akiwa na miaka 14 tu alipelekwa na baba yake Mathew Knowles studio lakini producer alipomsikia Beyonce akiimba alimwambia hadhani kama kuimba ni kipaji chake lakini leo hii Beyonce ni miongoni mwa waimbaji wakubwa duniani akiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekani Milioni 600 na kuuza zaidi ya rekodi milioni 34. 2: Shakira . Shakira ni miongoni mwa waimbaji wenye mafanikio makubwa dunia akiwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 220 na kuuza rekodi zaidi ya milioni 60 duniani kote lakini aliwahi kukataliwa kujiunga na kikundi cha kuimba kwaya kanisani na mwalimu wake wa muziki kumwambia ana sauti mbaya inayofanana na mbuzi...