Aliyoyasema Mwigulu Nchemba Kuhusu Mauwaji ya Askari Nane.
Mwigulu Nchemba baada ya kutembelea eneo walilouawa Askari Nane.
Wakati jioni ya April 13 2017 Wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, iliripotiwa kuwa watu wanaosadikika kuwa majambazi ambao haijafahamika idadi yao wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la polisi na kuwaua askari nane na kumjeruhi mmoja
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba leo April 14 2017 ametembelea eneo lilipotokea tukio la mauaji ya Askari nane wa Jeshi la Polisi na kusema kuwa waliotekeleza mauaji hayo watalipa damu ya akari hao iliyomwagika.
Comments