Jinsi ya Kurudisha Vitu vilivyofutwa au kupotea kwenye simu yako(Data Recovery).
JINSI YA KURUDISHA DATA ZAKO ZILIZOPOTEA KWENYE SIMU Njia Za Kupata Data Zako Zilizopotea (Zilizofutwa) Katika Kifaa Cha Android! Sio kitu kipya wote tumeshawahi fanya, kwa bahati mbaya tulishawahi kufuta taarifa zetu kama vile picha au hata video. Kama ikitokea hivyo tena usikasirike, TeknoKona inakuletea njia. Sawa kama nlivyosema kuwa unaweza ukapata taarifa zako zote ambazo ulifuta kwa bahati mbaya lakini kabla ya kuzipata kuna mambo inabidi uyafanye • Usihifadhi (save) kitu kingine chochote katika simu kifaa chako au izime mpaka ukiwa unampango wa kufufua vitu vyako • Zima WiFi na njia za mawasiliano za 2G/3G ili masashisho (update) ambayo huwa yanayofanyika automatiki yasifanyike . Kumbuka kama yakifanyika, mafaili mapya yanaweza jiweka juu ya yale ambayo unataka kutafufua Tuifahamu Njia Kama Mafaili Yako Yapo Katika Memori Kadi . Ukishaona mafaili yako yamefutika bahati mbaya – au hata kwa makusudi – kitu kinachofuata ni kuunganisha...