Tamko la Waziri Kuhusu Bonde la Mto Ruaha.

Tamko la waziri Makamba kuhusu bonde la Mto Ruaha.

Jumapili ya April 9 2017 waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais-muungano na mazingira January Makamba aliamua kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza mpango wake wa kuzindua kikosi kazi cha kitaifa kuhusu bonde la Mto Ruaha mkuu Iringa.

Mpango huo ambao makamu wa Rais na mawaziri watano wataelekea Iringa siku ya Jumanne ya April 11 2017 lengo likiwa ni kukagua na kuangalia bonde la mto Ruaha ambalo linakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira hususani wa ardhi.

Uharibifu wa mazingira katika bonde la mto Ruaha kwa kiasi kikubwa unatokana na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu zinazofanywa katika maeneo ya vyanzo vya maji pamoja na vilele vya milima, miteremko ya milima na katika mabonde.

Baada ya kugundua uharibifu huo unaoendelea kufanyika katika bonde la mto Ruaha, serikali kwa kushirikiana na wadau imeona kuna haja ya kuwa na mtazamo mpya wa namna ya kukabiliana na changamoto za mto Ruaha Mkuu kwa ufanisi zaidi.

Comments