Posts

Aliyoyasema Mwigulu Nchemba Kuhusu Mauwaji ya Askari Nane.

Mwigulu Nchemba baada ya kutembelea eneo walilouawa Askari Nane . Wakati jioni ya April 13 2017 Wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, iliripotiwa kuwa watu wanaosadikika kuwa majambazi ambao haijafahamika idadi yao wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la polisi na kuwaua askari nane na kumjeruhi mmoja Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba   leo April 14 2017 ametembelea eneo lilipotokea tukio la mauaji ya Askari nane wa Jeshi la Polisi na kusema kuwa waliotekeleza mauaji hayo watalipa damu ya akari hao iliyomwagika.

Maamuzi ya Canada Kuhusu Bangi Itakapofikia 2018 Ni haya.

Kufikia 2018 haya ndiyo maamuzi watakayofikia Canada kuhusu Bangi. Kadiri siku zinavyobadilika na miaka kusonga mbele ndivyo nchi mbalimbali duniani hufanya marekebisho katika sheria za nchi kulingana na hitajio la wananchi kwa maendeleo ya Taifa. Leo April 14, 2017 mtandao maarufu wa CNN umeripoti taarifa kuhusu mpango wa Serikali ya Canada chini ya Waziri Mkuu Justin Trudeau kuweka wazi mipango yake ya kuhalalisha bangi ifikapo 2018 ambapo kama Bunge la nchi hiyo litapitisha muswada huo, Canada itakuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kuhalalisha soko la bangi. Waziri Mkuu aliandika kwenye account yake ya Twitter: “ Ni rahisi sana kwa watoto wetu kupata bangi. Tutaibadilisha.“ – Justin Trudeau . Licha ya kutaka kuhalalisha bangi, pia yametajwa mambo matano ya kuyafahamu kuhusu pendekezo la Canada katika sera ya bangi ambayo rasmi itakuwa July 2018. 1: Serikali kusimamia mauzo ya bangi Serikali ya Canada itaweka mfumo maalum wa kuzalisha, kusambaza ...

Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Mauwaji ya Askari Nane.

Kauli ya Jeshi la Polisi kuhusu mauaji ya askari polisi nane . Jana April 13 2017 jioni Wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, iliripotiwa kuwa watu wanaosadikika kuwa majambazi ambao haijafahamika idadi yao wakiwa na silaha walishambulia kwa risasi gari la polisi na kuwaua askari nane na kumjeruhi mmoja. Leo April 14 2017 katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo , Nsato Marijani amesema katika tukio hilo majambazi hao walipora silaha saba ; SMG nne na Lon Range tatu. Aidha, Marijani amesema mara baada ya tukio hilo, hatua za kiintelijensia na kipelelezi ambazo zilichukuliwa askari kufuatilia, zilibaini maficho ya muda ya majambazi hao ambapo katika majibizano ya risasi majambazi wanne waliuawa na bunduki nne kupatikana hivyo amesema kuanzia sasa Jeshi la Polisi linakwenda kwenye oparesheni maalumu kupambana na majambazi hao.

Raisi John P.Magufuli Ampigia Simu Nwana FA na Kumpongeza.

Image
Jioni ya April 12 2017 staa wa muziki wa hip hop bongo Hamisi Mwinjuma ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la Mwana FA, alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuoneshwa kufurahisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kumpigia simu. Mwana FA ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika radio na tv stations mbambali kwa hit single yake ya Dume Suruali amethibitisha kupigiwa simu na Rais kumwambi anakubali kazi zake. Kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa staa huyo uliyokuwa verified aliandika “nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais @ MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa # DumeSuruali ..

Serikali yatangaza majina ya Ajira za Ualimu.

BREAKING NEWS: HAYA HAPA MAJINA AJIRA MPYA ZA WALIMU 2016/2017. Hatimaye serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza majina ya walimu walioajiriwa mwaka katika Ngazi ya Stashahada wa Mwaka 2016/2017           Bonyeza hapa kuyatazama .

Walicholisema Stamina na Bill Bass kuhusiana na utekaji huku wakiitambulisha Ngoma Yao Mpya.

Stamina na Bill Nass wamezungumzia kuhusu utekaji . Leo April 12 2017 kupitia kwenye XXL ya Clouds FM wakali kutoka Bongoflevani Bill Nass na Stamina wamezungumzia kuhusu vitendo vya utekaji watu baada ya Roma Mkatoliki na wenzake watatu kutekwa na watu wasiojulikana kabla ya kuonekana. Stamina amedai kuwa haoni sababu nyingine zaidi ya muziki ambao umekuwa hukisababisha utekaji hivyo kuwanyima uhuru wa sanaa, huku Bill Nass akisema hatumii muda mwingi kutoka nje kabla na  baada ya saa sita usiku kuhofia kutekwa. >>>“ Sioni kama kuna kitu kingine zaidi ya muziki. Ndiyo sababu nayaona matukio ya utekaji kama ni kutunyima uhuru wa sanaa yetu ." - Stamina . >>>” Siku hizi situmii muda mwingi nje. Watu wangu wa karibu wanapenda niwepo ndani kabla ya saa sita usiku juu ya hofu ya utekaji. ” - Billnass . Bill Nass na Stamina wamezitoa kauli hizo wakati wakiutambulisha wimbo wao mpya unaoitwa Aje mwenyewe walioshirikiana wasa...

RFEF Imemfungia Neymar Mechi tatu mfululizo.

BAD NEWS: RFEF imemfungia Neymar leo April 11 2017. Staa wa soka wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Neymar amekutana na adhabu ya kufungiwa mechi 3 mfululizo  kuichezea FC Barcelona na shirikisho la soka Hispania ( Royal Spanish Football Federation (RFEF) kwa makosa mawili. Neymar amefungiwa mechi tatu, mechi moja ni kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano wakati wa mchezo dhidi ya Malaga uliyomalizika kwa FC Barcelona kupoteza kwa magoli mawili kwa 2-0 lakini mechi ya mbili kwa kosa la kumpongeza kwa kejeli fourth official wakati anatoka nje ya uwanja. Neymar alipooneshwa kadi ya pili ya njano, Mchezaji huyo raia wa Brazil alitoa lugha za kejeli kwa fourth official wakati anatoka uwanjani kwa kuoneshwa kadi ya pili ya njano, refa wa game hiyo Jesus Gil Manzano ndio aliandika ripoti hiyo, Neymar sasa atakosa mchezo dhidi ya Real Sociedad, Real Madrid na Osasuna.

Wajumbe Walioapishwa na Mheshimiwa Raisi ili kwenda kufanya Uchunguzi wa Makontena yaliotoka nchini Tangu Mwaka 1998.

Rais Maghufuli amewaapisha Wajumbe wa Kamati Maalumu . Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo April 11, 2017 amewaapisha Wajumbe wa Kamati Maalum ya pili ya wachumi na wanasheria ambayo itachunguza mchanga wenye madini uliomo kwenye makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini. Wajumbe walioapishwa ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Nehemiah Eliachim Osoro na wajumbe wake ambao ni Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara, Dkt. Oswald Joseph Mashindano, Bw. Casmir Sumba Kyuki, Bw. Andrew Wilson Massawe na Bw. Gabriel Pascal Malata . Wengine ni Bw. Usaje Bernard Usubisye na Bi. Butamo Kasuka Philip ambapo baada ya kuwaapisha wajumbe hao Rais Magufuli amesema ameunda kamati hiyo ili ifanye uchunguzi wa kina utakaobaini aina ya madini yaliyomo ndani ya mchanga huo, thamani yake, kiwango cha kila aina ya madini, uzito wa mchanga unaowekwa ndani ya makontena na kujua ni makontena mangapi yamepitishwa tangu mwaka 1998. “ Kafuatilieni makontena mangapi yametoka hapa nchini na kupe...

Sifa za wanaotakiwa kujiunga na Mafunzo ya Afya Ngazi ya Cheti na Stashahada(Diploma).

Kwa wale wanaohitaji kutumq mombi kwa ajili ya mafunzo ingia link hii hapa chini ili kuweza kutazama Sifa za waombaji mafunzo ya Afya katika Ngazi za Cheti na Stashahada yaani Diploma. http:// maswayetu.blogspot.nl /2017/04/ taarifa-muhimu-kuhusu-sifa-za-kujiunga.html .

Viwanja Kumi Bora Afrika,Ukanda wa Mashariki Upo mmoja tu.

TOP 10 ya viwanja ghali zaidi Afrika , Afrika Mashariki upo mmoja . Licha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF kusema moja ya sababu kuu inayopelekea Bara la Africa kufanya vibaya kwenye mchezo wa mpira wa miguu duniani ni ukosefu wa viwanja bora, kuna baadhi ya nchi Afrika zina viwanja vizuri na vyenye gharama kubwa ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea. Leo April 10, 2017 nimekuletea list ya viwanja 10 vizuri na vyenye gharama zaidi barani Afrika hadi kufikia December 2016. 1: Capetown Stadium, Afrika Kusini Uwanja huu una uwezo wa kuingiza mashabiki 64,100 ambapo umejengwa na kampuni ya Afrika Kusini ukiigharimu nchi hiyo Dollar 600 million ukiwa ndiyo uwanja wenye gharama kwa Afrika. 2: Moses Madiba Stadium, Afrika Kusini Moses Madiba ulikuwa moja ya viwanja vilivyotumika wakati wa Fainali za Kombe la Dunia 2010 ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya 62,760. Uligharimu Dollar 450 million. 3: FNB Stadium, Afrika Kusini Uwanja huu unashikilia rekodi ya...

Tamko la Waziri Kuhusu Bonde la Mto Ruaha.

Tamko la waziri Makamba kuhusu bonde la Mto Ruaha . Jumapili ya April 9 2017 waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais-muungano na mazingira January Makamba aliamua kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza mpango wake wa kuzindua kikosi kazi cha kitaifa kuhusu bonde la M to Ruaha mkuu Iringa . Mpango huo ambao makamu wa Rais na mawaziri watano wataelekea Iringa siku ya Jumanne ya April 11 2017 lengo likiwa ni kukagua na kuangalia bonde la mto Ruaha ambalo linakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira hususani wa ardhi. Uharibifu wa mazingira katika bonde la mto Ruaha kwa kiasi kikubwa unatokana na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu zinazofanywa katika maeneo ya vyanzo vya maji pamoja na vilele vya milima, miteremko ya milima na katika mabonde. Baada ya kugundua uharibifu huo unaoendelea kufanyika katika bonde la mto Ruaha, serikali kwa kushirikiana na wadau imeona kuna haja ya kuwa na mtazamo mpya wa namna ya kukabiliana na changamoto za mto Ruaha Mkuu kwa ufa...

Lau Wa John Feat Lee Classic & Zilly-Usijari.

Sikiliza wimbo mpya kutoka kwa Lau wa John Feat Lee Classic & Zilly- Usijari . Bofya hapa chini kuupakua na kuusikiliza pia. http://www.djmwanga.com/2017/03/lau-wa-john-x-lee-classic-x-zilly-usijari.html?m=1

To those who wants to Make and Earn Money Online.

Please follow the Link below in order to be directed on how to get paid when you share your link with your family members. http:// dollarsaw.com /?share=154803 Usikose kutembelea www . dbmclassic . blogspot . com / Kila mara ili kupata taarifa mbalimbali.

Nchi Ishirini Zinazoongoza kwa Mabilionea.

DUNIANI TOP 20 ya nchi zenye Mabilionea wengi zaidi Duniai . Baada ya Shirika la Fedha duniani ‘IMF’ kutangaza kuongezeka kwa uchumi wa dunia ukilinganisha na mwaka 2016, taarifa iliyoweza kutolewa April 8 2017 ikionesha list ya nchi zenye mabilionea wengi zaidi duniani kwa mwaka 2017, kwa mujibu wa tovuti ya takwimu Statista . Takwimu hizi zinaonesha kuwa;- 1.China ndiyo nchi yenye mabilionea wengi duniani ambao ni zaidi ya 609. 2.kifuatiwa na Marekani yenye mabilionea 552. 3.Ujerumani-109. 4.India-100. 5.Uingereza-89. 6.Uswizi-77. 7.Urusi-68. 8.Ufaransa-50. 9.Brazili-43. 10.Japani-42. 11.Italia-41. 12.Kanada-35. 13.Korea Kusini-34. 14.Uturuki-29. 15.Singapo-28. 16.Australia-27. 17.Tailendi-26. 18.Hispania-23. 19.Jamhuri ya Nchi za Kiarabu(U.A.E)-21. 20.Indonesia-17. Katika list hii Sweden inakamata nafasi ya mwisho ikiwa na mabilionea 17.

Roma, three Colleagues found Bruised (Strike):Lawyer.

Roma, three colleagues found bruised: lawyer . Hip hop star Ibrahim Musa a.k.a Roma Mkatoliki . @TheCitizenTz. Dar es Salaam. Hip hop star Ibrahim Musa a.k.a Roma Mkatoliki and his three colleagues who went missing on Wednesday evening after a suspected abduction were yesterday found alive in undisclosed locations and circumstances. Speaking from Mwananyamala Referral Hospital where he and the three had been taken for treatment, Roma said : “I thank Tanzanians for their support. I’m well but I can’t talk more for now. I’m waiting for police procedures. ” He promised to hold a press conference tomorrow and divulge details ". By noon yesterday, Dar es Salaam Special Zone police commander Simon Sirro told the press that the whereabouts of Roma and his colleagues was unknown. However, about an hour later, it came to light that the artistes had been found and were at the Oysterbay Police Station. However, journalists were barred from interviewing them a...

Roma Aongea kwa mara ya lwanza baada ya kurudi Uraiani.

MIX VIDEO: Roma aongea kwa mara ya kwanza baada ya kurudi uraiani By Millard Ayo. Msanii wa Bongofleva Roma Mkatoliki na wenzake watatu wamerudi uraiani baada ya kuripotiwa kutekwa April 5 2017 na kupelekwa kusikojulikana, baada ya kurudi uraiani ameyaongea haya hapa chini. " Siwezi kuongea mengi maana tunahitaji muda wa kupumzika nopende kuwaambia watanzania wote mimi ni mzima pamoja na wenzangu wote watatu Moni , Emma na Bin Laden hivyo pia nipende kuwashukuru watanzania wote kwa support yao japokuwa sijaweza kupita katika mitandao ya kijamii pia niweze lumshukuru ndugu Ruge Mtaaba kwa ushirikiano wake tangu asubuhi tumekuwa naye "

Breaking News.

Taarifa zilizopo zinazohusu Roma alipo . Taarifa ambazo zimetolewa leo mchana na mmiliki wa Studio ya TONGWE zinasema kuwa Roma na wenzake ambao waliotekwa wameweza kujulikanaahali walipo amnapo ameweza kutaja kuwa Roma na wenzake wapo katika kituo cha Osterbay . Taarifa zaidi nitakusogezea kila inapotokea mahali au sehemu yoyote ahsante.

Alichokiandika Mbunge Hessein Bashe kuhusu Roma Mkatoliki.

Alichokiandika Mbunge Hussein Bashe kuhusu Roma Mkatoliki By Rama Mwelondo . TZA . Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatoliki zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuripotiwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa Studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana. Watu mbalimbali ikiwemo wasanii mbalimbali wamekuwa wakionesha hisia zao juu ya tukio hilo kwa kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuoneshwa kuguswa na tukio hilo, Mbunge wa Nzega Hussein Bashe ni miongoni mwa watu waliyotumia kuraza zao za instagram kuandika anachowaza kuhusu Roma. Who is behind all this? “ Ni genge ambalo limejipa mamlaka ya kupandikiza woga na chuki miongoni mwa jamii na kuharibu Taswira ya CCM. Tunawajibu wa kukataa woga ,Tunawajibu wa kutoruhusu Misuse ya vyombo vya Ulinzi na usalama, Tunawajibu wa kulinda Taifa letu ” “ Tunawajibu wa kupigania Values zilizopiganiwa na waasisi wa Tai...

Maneno Matatu ya Nape Kuhusu kutokuonekana kwa Roma.

Maneno matatu ya Nape Nnauye kuhusu Roma . Baada ya mastaa mbalimbali kuguswa juu ya stori ya Roma mkatoliki na wenzake watatu kuchukuliwa na watu wasiofahamika kwenye Studio za Tongwe Records na kupelekwa sehemu isiyojulikana, sasa leo April 7 2017 Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Moses Nnauye ameonesha hisia zake juu ya tukio hilo. Kupitia account yake ya twitter Nape Nnauye ameyaandika maneno haya matatu kuhusu Roma…>>> ”Roma! Oooooh No! ” -Nape Nnauye.

The Siti Msanii kutoka TONGWE alivyoshuhudia kuchukuliwa kwa Roma.

Shuhuda ameeleza Roma na wenzake walivyochukuliwa Tongwe Records. Zimepita siku mbili tangu staa wa Hip Hop Bongo Roma kuchukuliwa na watu wasiojulikana pamoja na wenzake wakiwa katika studio za Tongwe Records bila kujulikana walikopelekwa, basi leo April 7, 2017 msanii kutoka Tongwe Records ameelezea jinsi watu hao walivyochukuliwa. The Siti ameiambia millardayo.com na Ayo TV jinsi Roma Mkatoliki na wenzake walivyochukuliwa Tongwe Records ambapo hadi sasa haijafahamika mahala walipo na watu waliowachukua . Akizungumza na millardayo.com pamoja na  Ayo TV The Siti alisema:>>> ”Ilitokea kama Jumatano saa kumi na mbili jioni na walikuja watu pale wakashuka kutoka kwenye Noah wakatuambia tuingie ndani ya geti na tukaingia ndani ya geti. Wakamuulizia Junior wakaambiwa hayupo, kisha wakamuulizia na Roma Mkatoliki wakaomba waitiwe Roma kisha walipoitiwa Roma, walimuhoji pale mara wakaingia studio wakachukua vitu na wakawachukua wakina Moni .” -The Siti...