NAMNA YA KUACHA KUPIGA PUNYETO {KUJICHUA} KWA WANAUME NA WANAWAKE. Hebu niambie, umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Najua unaona aibu, hasa kama una tabia hiyo. Usiogope rafiki yangu, leo nitazungumza na wewe taratibu halafu mwisho kabisa nitakuacha na tabasamu la nguvu! Ndugu zangu, wakati mwingine kuna mambo magumu kidogo ambayo baadhi ya watu wanayaonea aibu, lakini yanaendelea kuwa tatizo kwa watu wengi. Leo tutazungumza. Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo, hawapendi hata kidogo. Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha, lakini baada ya saa kadhaa kupita, wanarudi kule kule. Kama una tabia hiyo, utakuwa unanielewa vizuri zaidi juu ya kile ninachokizungumzia hapa. Hebu twende tukaone. KUJICHUA NI NINI HASA ? Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa ‘masturbation’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rah...