Donald Trump Atetea kuhusu Mkutano na Wakili wa Urusi aliyedai kuwa Taarifa kumhusu Hillary Clinton.
Trump Junior atetea mkutano na wakili wa Urusi aliyedai kuwa na taarifa kumhusu Hillary Clinton.
Trump Jr anasisitiza kuwa wakili huyo hakutoa taarifa muhimu kumhusu Bi H. Clinton
Mtoto wa kiume wa Rais wa Marekani Donald Trump amevishambulia vyombo vya habari kufuatia madai ya mkutano na wakili mrusi ambaye alisema kuwa alikuwa na habari za kumchafulia jina Hillary Clinton.
Donald Trump Jr amekana kutoa habari za kukanganya kuhusu mkutano huo wa mwaka uliopita.
Pia amesema kuwa lilikuwa jambo la kawaida kupata taarifa kuhusu wagombea pinzani.
Donald Trump junior alifanya mkutano na wakili wa Urusi,Maafisa nchini Marekani wanachunguza madai yanayohusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Mkwe wa Trump Jared Kushner na aliyekuwa mkuu wa kampeni Paul J Manafort, walikuwa pia katika mkutano huo na Natalia Veselnitskaya.
Jared Kushner hajazungumza kuhusu taarifa ya Donald Trump Jr
Trump Jr anasisitiza kuwa wakili huyo hakutoa taarifa muhimu kumhusu Bi Clinton, ambaye alikuwa mshindani wa babake katika kiti cha urais.
Mkutano huo ulifanyika tarehe 9 mwezi Juni mwaka 2016 katika jengo la Trump Tower, wiki mbili baada ya Donald Trump kupata uteuzi wa Republican.
Trump Junior alikutana na wakili wa Urusi
Unaaminiwa kuwa mkutano wa kwanza wa siri kati ya raia wa Urusi na watu waliokuwa karibu na Bwana Trump.
Baada ya New York Times kuripoti mara ya kwanza kuhusu mkutano huo siku ya Jumamosi, Bwana Trump Jr alitoa taarifa iliyothibitisha kuwa mkutano huo ulifanyika lakini haikutaja ikiwa ulihusu kampeni ya kuwania urais.
Comments