Popular posts from this blog
Wasanii Waliowahi Kuambiwa hawajui kuimba lakini sasa ni Mastaa.
BURUDANI Waimbaji 10 waliowahi kuambiwa hawajui kuimba lakini leo ni mastaa wa Dunia. Mara nyingi watu wanaposhindwa na jambo hukata tamaa lakini kushindwa mara moja haimaanishi huwezi kufanikiwa jambo hilo ukijaribu tena na tena, leo nimekuletea list ya wanamuziki kumi waliowahi kuambiwa hawajui kuimba na leo hii ni mastaa wakubwa duniani. 1: Beyonce . Akiwa na miaka 14 tu alipelekwa na baba yake Mathew Knowles studio lakini producer alipomsikia Beyonce akiimba alimwambia hadhani kama kuimba ni kipaji chake lakini leo hii Beyonce ni miongoni mwa waimbaji wakubwa duniani akiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekani Milioni 600 na kuuza zaidi ya rekodi milioni 34. 2: Shakira . Shakira ni miongoni mwa waimbaji wenye mafanikio makubwa dunia akiwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 220 na kuuza rekodi zaidi ya milioni 60 duniani kote lakini aliwahi kukataliwa kujiunga na kikundi cha kuimba kwaya kanisani na mwalimu wake wa muziki kumwambia ana sauti mbaya inayofanana na mbuzi...
The Siti Msanii kutoka TONGWE alivyoshuhudia kuchukuliwa kwa Roma.
Shuhuda ameeleza Roma na wenzake walivyochukuliwa Tongwe Records. Zimepita siku mbili tangu staa wa Hip Hop Bongo Roma kuchukuliwa na watu wasiojulikana pamoja na wenzake wakiwa katika studio za Tongwe Records bila kujulikana walikopelekwa, basi leo April 7, 2017 msanii kutoka Tongwe Records ameelezea jinsi watu hao walivyochukuliwa. The Siti ameiambia millardayo.com na Ayo TV jinsi Roma Mkatoliki na wenzake walivyochukuliwa Tongwe Records ambapo hadi sasa haijafahamika mahala walipo na watu waliowachukua . Akizungumza na millardayo.com pamoja na Ayo TV The Siti alisema:>>> ”Ilitokea kama Jumatano saa kumi na mbili jioni na walikuja watu pale wakashuka kutoka kwenye Noah wakatuambia tuingie ndani ya geti na tukaingia ndani ya geti. Wakamuulizia Junior wakaambiwa hayupo, kisha wakamuulizia na Roma Mkatoliki wakaomba waitiwe Roma kisha walipoitiwa Roma, walimuhoji pale mara wakaingia studio wakachukua vitu na wakawachukua wakina Moni .” -The Siti...
Comments