Shilingi milioni 40.4 za kashfa ya Escrow zarejeshwa Tanzania . Mbunge wa Sengerema na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja , akiongea na wanahabari ambao hawako pichani, leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam . Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Habari Bi . Zamaradi Kawawa . YAH: KURUDISHA FEDHA (TZS MILIONI 40.4) NILIZOPEWA NA NDUGU JAMES RUGEMALIRA WA KAMPUNI YA VIP ENGINEERING AND MARKETING LTD. 1. Kama inavyokumbukwa, kutokana na ukweli kwamba ilisharipotiwa sana kwenye vyombo vya habari, kwamba tarehe 12/02/2014 nilipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 40.4 za kitanzania kutoka kwa Ndugu James Rugemalira , mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd. Fedha hizo nilizipokea kupitia akaunti yangu namba 00110102352601 ya Benki ya Mkombozi . 2. Fedha hizo nilizipokea, kwa nia njema, kama msaada/mchango kutoka kwa ndugu Rugemalira ili zinisaidie katika kutimiza majukumu yangu ya kibunge, hususan,kusaidiana na wa...